Zaburi 41:7-10
Zaburi 41:7-10 SRUV
Wote wanaonichukia wananong'onezana juu yangu, Wananiwazia yaliyo mabaya zaidi. Wanafikiri pigo liualo limemshika, Akalala asiweze kusimama tena. Hata rafiki yangu mwandani niliyemtumaini, Aliyekula pamoja nami, Ameniinulia kisigino chake. Lakini Wewe, BWANA, unifadhili, Uniinue nipate kuwalipa.