Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 119:25-32

Zaburi 119:25-32 SRUV

Nafsi yangu imegandamia mavumbini, Unihuishe sawasawa na neno lako. Nilizisimulia njia zangu ukanijibu, Unifundishe amri zako. Unifahamishe njia ya maagizo yako, Nami nitayatafakari maajabu yako. Nafsi yangu imeyeyuka kwa huzuni, Unitie nguvu sawasawa na neno lako. Uniondolee njia ya uongo, Unineemeshe kwa sheria yako. Nimeichagua njia ya uaminifu, Na kuziweka hukumu zako mbele yangu. Nimeambatana na shuhuda zako, Ee BWANA, usiniaibishe. Nitakwenda mbio katika njia ya maagizo yako, Utakaponipanulia ufahamu wangu.

Soma Zaburi 119

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha