Luka 22:63-71
Luka 22:63-71 SRUV
Na wale watu waliokuwa wakimshika Yesu walimfanyia dhihaka, wakampiga. Wakamfunika macho, kisha wakamwulizauliza wakisema, Tabiri, ni nani aliyekupiga? Wakamtolea na maneno mengine mengi ya kumtukana. Kulipokucha, walikutanika jamii ya wazee, na wakuu wa makuhani, na waandishi, wakamleta katika baraza yao, wakisema, Kama wewe ndiwe Kristo, tuambie. Akawaambia, Nikiwaambia, hamtasadikia. Tena, nikiwauliza, hamtajibu. Lakini tangu sasa Mwana wa Adamu atakuwa ameketi upande wa kulia wa Mungu Mwenyezi. Wakasema wote, Basi, wewe ndiwe Mwana wa Mungu? Akawaambia, Ninyi mwasema kwamba mimi ndiye. Wakasema, Basi, tuna haja gani tena ya ushuhuda? Maana, sisi wenyewe tumesikia maneno ya kinywa chake.