Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mambo ya Walawi 6

6
1 # Hes 5:5-8 BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 2#Hes 5:6; Law 19:11; Mdo 5:4; Kol 3:9; Kut 22:7,10; Mit 24:28; 26:19 Mtu awaye yote akifanya dhambi, na kuasi juu ya BWANA, akamdanganya mwenziwe katika jambo la amana, au la mapatano, au la kunyang'anya, au kumwonea mwenziwe; 3#Kum 22:1; Law 19:12; Yer 7:9; Zek 5:4; Kut 22:11 au kupata kitu kilichopotea na kutenda la uongo juu yake, na kuapa kwa uongo; katika mambo hayo yote mojawapo atakalolitenda mtu, na kufanya dhambi kwalo; 4ndipo itakapokuwa, akiwa amefanya dhambi, na kupata hatia, atarudisha hicho alichokipata kwa kunyang'anya, au kitu kile alichokipata kwa kuonea, au ile amana aliyowekewa, au kitu kile kilichopotea alichokipata yeye, 5#Law 5:16; Hes 5:7; 2 Sam 12:6; Lk 19:8 au kitu chochote ambacho amekiapia uongo; atakirudisha hata kwa utimilifu wake, kisha ataongeza na sehemu ya tano zaidi juu yake; naye atampa huyo mwenyewe, siku hiyo ambayo atakapohukumiwa kuwa mwenye hatia. 6#Kut 12:5; Law 3:1; 22:20; Kum 15:21; Mal 1:14; Efe 5:27; 1 Tim 2:5,6; Ebr 9:14; 10:1-17 Kisha ataleta sadaka yake ya hatia kwa BWANA, ni kondoo dume wa katika kundi lake, mkamilifu, sawasawa na hesabu utakayomwandikia, kuwa sadaka ya hatia, na kumpa kuhani; 7na huyo kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele za BWANA, naye atasamehewa; katika jambo lolote alifanyalo hata akapata kuwa mwenye hatia kwalo.
Mafunzo kuhusu kafara
8BWANA akanena na Musa na kumwambia, 9Haya, mwagize Haruni na wanawe, uwaambie, Amri ya sadaka ya kuteketezwa ni hii; hiyo sadaka ya kuteketezwa itakuwa pale motoni juu ya madhabahu usiku wote hadi asubuhi; na huo moto wa madhabahu utawaka juu yake usizimike. 10#Law 16:4; Kut 28:39-43; Eze 44:17 Naye kuhani atavaa nguo yake ya kitani, na suruali zake za kitani atazivaa mwilini mwake; naye atayazoa majivu ambayo huo moto umeiteketezea sadaka juu ya madhabahu, kisha atayaweka kando ya madhabahu. 11Kisha atayavua mavazi yake, na kuvaa mavazi mengine, kisha atayachukua yale majivu kwenda nayo nje ya kambi hata mahali safi. 12Na huo moto ulio madhabahuni atautunza uwake daima juu yake, usizimike; naye kuhani atateketeza kuni katika moto huo kila siku asubuhi; naye ataipanga sadaka ya kuteketezwa juu yake, naye atayateketeza mafuta ya sadaka za amani juu yake. 13#Zab 50:3; Isa 33:14; Dan 7:10; Mt 25:41 Moto utatunzwa uwake juu ya madhabahu daima; usizimike.
14 # Hes 15:4 Na amri ya hiyo sadaka ya unga ni hii; wana wa Haruni wataisongeza mbele za BWANA, mbele ya madhabahu. 15Naye atatwaa konzi yake katika huo unga, katika huo unga mwembamba wa sadaka ya unga, na katika mafuta yake, na ubani wote ulio juu ya sadaka ya unga, kisha atauteketeza juu ya madhabahu kuwa harufu ya kupendeza, kuwa ukumbusho wake kwa BWANA. 16#Hes 18:10 Na unga uliosalia Haruni na wanawe wataula; utaliwa pasipo kutiwa chachu, katika mahali patakatifu; katika ua wa hema ya kukutania ndipo watakapoula. 17#Law 2:11; Hes 18:9,10; Kut 29:37 Hautaokwa kwa chachu. Nimewapa kuwa sehemu yao katika matoleo yangu yasongezwayo kwa njia ya moto; ni kitu kitakatifu sana, kama hiyo sadaka ya dhambi, na kama hiyo sadaka ya hatia. 18#Hes 18:10; Law 3:17; 22:3; Kut 29:37 Kila mwanamume miongoni mwa wana wa Haruni atakula katika huo, kuwa ni haki yao milele katika vizazi vyenu, katika matoleo ya BWANA yasongezwayo kwa njia ya moto; mtu yeyote atakayevigusa atakuwa ni mtakatifu.
19BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 20#Kut 29:2; 16:36 Matoleo ya Haruni na wanawe watakayomtolea BWANA, katika siku atakayotiwa mafuta, ni haya; sehemu ya kumi ya efa ya unga mwembamba kuwa sadaka ya unga daima, nusu yake asubuhi, na nusu yake jioni. 21Utaandaliwa kikaangoni pamoja na mafuta; ukisha kulowama utauleta ndani; utasongeza hiyo sadaka ya unga vipande vilivyookwa, iwe harufu ya kupendeza kwa BWANA. 22#Kut 29:25; Isa 53:10; Mt 20:28; Dan 9:26; 1 Tim 2:6 Na huyo kuhani aliyetiwa mafuta badala yake katika hao wanawe ataisongeza; itateketezwa kabisa kwa BWANA kwa amri ya milele. 23Tena kila sadaka ya unga ya kuhani itateketezwa kabisa; isiliwe.
24BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 25#Law 4:24,29; 21:22; Zab 93:5 Nena na Haruni na wanawe, uwaambie, Amri ya hiyo sadaka ya dhambi ni hii; mahali hapo pachinjwapo sadaka ya kuteketezwa ndipo itakapochinjwa sadaka ya dhambi, mbele za BWANA; ni takatifu sana. 26#Hes 18:9; Eze 44:27,28 Huyo kuhani atakayeisongeza kwa ajili ya dhambi ndiye atakayeila; italiwa katika mahali patakatifu, katika ua wa hema ya kukutania. 27#Kut 29:37; 30:29 Kila kitu kitakachoigusa nyama ya sadaka hiyo kitakuwa kitakatifu; tena itakapomwagika damu yake yeyote katika nguo yoyote, utaifua nguo hiyo iliyomwagiwa, katika mahali patakatifu. 28#Law 11:33; 15:12 Lakini hicho chombo cha udongo ambacho hiyo nyama ilipikwa ndani yake kitavunjwa; na kama ikipikwa katika chombo cha shaba, kitasuguliwa, na kuoshwa kwa maji. 29#Hes 18:10 Kila mwanamume miongoni mwa makuhani atakula katika hiyo; ni takatifu sana. 30#Law 16:27; Ebr 13:11 Wala haitaliwa sadaka ya dhambi yoyote, ambayo damu yake yoyote ililetwa ndani ya hema ya kukutania, ili kufanya upatanisho katika mahali patakatifu; itateketezwa.

Iliyochaguliwa sasa

Mambo ya Walawi 6: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha