Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yohana 13:21-25

Yohana 13:21-25 SRUV

Naye alipokwisha kusema hayo, Yesu alifadhaika rohoni, akashuhudia akisema, Amin, amin, nawaambieni, Mmoja wenu atanisaliti. Wanafunzi wakatazamana, huku wakiwa na mashaka ni nani amnenaye. Na palikuwapo mmoja wa wanafunzi wake, ameegama kifuani pa Yesu, ambaye Yesu alimpenda. Basi Simoni Petro akampungia mkono, akamwambia, Uliza, ni nani amtajaye? Basi yeye, huku akimwelekea Yesu kifua chake, akamwambia, Bwana, ni nani?

Soma Yohana 13