1 Samweli 20:16-18
1 Samweli 20:16-18 SRUV
Basi Yonathani akafanya agano na jamaa yake Daudi, akisema, BWANA na awalipize kisasi adui zake Daudi. Naye Yonathani akamwapisha Daudi mara ya pili, kwa ajili ya upendo aliokuwa nao kwake; kwa maana alimpenda kama alivyoipenda roho yake mwenyewe. Kisha Yonathani akamwambia, Kesho ni mwandamo wa mwezi, nawe utakosekana, kwa sababu kiti chako kitakuwa hakina mtu.