Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yohana 17

17
Yesu awaombea wanafunzi wake
1 # Yn 11:14; 13:1 Maneno hayo aliyasema Yesu; akainua macho yake kuelekea mbinguni, akasema, Baba, saa imekwisha kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako naye akutukuze wewe; 2#Mt 11:27 kama vile ulivyompa mamlaka juu ya watu wote,#17:2 au wote wenye mwili. ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele. 3#1 Yoh 5:20; 1 The 1:9 Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma. 4#Yn 4:34 Mimi nimekutukuza duniani, nikiwa nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye. 5#Yn 1:1; 17:24; Flp 2:6 Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako. 6#Yn 17:9; Mt 6:9 Jina lako nimewadhihirishia watu wale ulionipa katika ulimwengu; walikuwa wako, ukanipa mimi, na neno lako wamelishika. 7Sasa wamejua ya kuwa yote uliyonipa yatoka kwako. 8#Yn 16:30 Kwa kuwa maneno uliyonipa nimewapa wao; nao wakayapokea, wakajua hakika ya kuwa nilitoka kwako, wakasadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma. 9#Yn 6:37,44 Mimi nawaombea hao; siuombei ulimwengu; bali hao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako; 10#Yn 16:15; Lk 15:31 na wote walio wangu ni wako, na walio wako ni wangu; nami nimetukuzwa ndani yao.
11 # Yn 10:30; Mt 6:13 Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo. 12#Zab 41:9; 109:8; Yn 13:18; 6:39; 2 The 2:3 Nilipokuwapo pamoja nao, mimi niliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie. 13#Yn 15:11 Na sasa naja kwako; na maneno haya nayasema ulimwenguni, ili wawe na furaha yangu imetimizwa ndani yao. 14#Yn 15:19 Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. 15#2 The 3:3; 1 Yoh 5:18; Mt 6:13; Lk 22:32 Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu. 16Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. 17#Yn 6:63 Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli. 18#Yn 20:21 Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo niliwatuma hao ulimwenguni. 19#Ebr 10:10 Na kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe, ili na hao watakaswe katika kweli.
20 # Yn 17:9 Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao. 21#Gal 3:28 Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma. 22#Mdo 4:32 Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja. 23#1 Kor 6:17; Gal 2:20 Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi. 24#Yn 10:29; 12:26; Efe 1:4 Baba, hao ulionipa nataka wawe pamoja nami popote nilipo, wapate na kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa msingi ulimwengu. 25Baba mwenye haki, ulimwengu haukukujua; lakini mimi nilikujua, na hao wamejua ya kuwa ndiwe uliyenituma. 26Nami niliwajulisha jina lako, tena nitawajulisha hilo; ili pendo lile ulilonipenda mimi liwe ndani yao, nami niwe ndani yao.

Iliyochaguliwa sasa

Yohana 17: SRUVDC

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha