Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 94

94
Mungu Amlipiziaye Mwenye Haki
1Ee BWANA, Mungu wa kisasi,
Mungu wa kisasi, uangaze,
2 # Mwa 18:25 Mwenye kuihukumu nchi, ujitukuze,
Uwape wenye kiburi stahili zao.
3 # Ayu 20:5 BWANA, hata lini wasio haki,
Hata lini wasio haki watashangilia?
4 # Yud 1:15 Je! Wote watendao uovu watatoa maneno,
Na kusema majivuno, na kufanya kiburi?
5Ee BWANA, wanawaseta watu wako;
Wanautesa urithi wako;
6Wanamwua mjane na mgeni;
Wanawafisha yatima.
7Nao husema, BWANA haoni;
Mungu wa Yakobo hafikiri.
8Enyi wajinga miongoni mwa watu, fikirini;
Enyi wapumbavu, lini mtakapopata akili?
9 # Kut 4:11; Mit 20:12 Aliyelitia sikio mahali pake asisikie?
Aliyelifanya jicho asione?
10 # Ayu 35:11; Yn 6:45; Isa 2:3; 28:26 Awaadibuye mataifa asikemee?
Amfundishaye mwanadamu asijue?
11 # 1 Kor 1:21; 1 Kor 3:20 BWANA anajua mawazo ya mwanadamu,
Ya kuwa ni ubatili.
12 # Ayu 5:17; Mit 3:11; 1 Kor 11:32 Ee BWANA, heri mtu yule umwadibuye,
Na kumfundisha kwa sheria yako;
13Upate kumstarehesha siku za mabaya,
Hata asiye haki atakapochimbiwa shimo.
14 # Kum 31:6; 1 Sam 12:22; 1 Fal 6:13; Yer 31:37 Kwa kuwa BWANA hatawatupa watu wake,
Wala hutauacha urithi wake,
15Maana hukumu itairejea haki,
Na wote walio wanyofu wa moyo wataifuata.
16Ni nani atakayesimama
Kwa ajili yangu juu ya wabaya?
Ni nani atakayenisaidia
Juu yao wafanyao maovu?
17Kama BWANA asingalikuwa msaada wangu,
Nafsi yangu kwa upesi ingalikaa penye kimya.
18Niliposema, Mguu wangu unateleza;
Ee BWANA, fadhili zako zilinitegemeza.
19Katika wingi wa mawazo ya moyoni mwangu,
Faraja zako zaifurahisha roho yangu.
20 # Amo 6:3; 2 Kor 6:14; Zab 58:2; Isa 10:1 Je! Kiti cha udhalimu kishirikiane nawe,
Kitungacho madhara kwa njia ya sheria?
21 # Mt 27:1; Kut 23:7; Mit 17:15 Huishambulia nafsi yake mwenye haki,
Na kuihukumu damu isiyo na hatia.
22Lakini BWANA amekuwa ngome kwangu,
Na Mungu wangu mwamba wangu wa kukimbilia.
23 # Mit 2:22 Naye atawarudishia uovu wao,
Atawaangamiza katika ubaya wao,
Naam, BWANA, Mungu wetu, atawaangamiza.

Iliyochaguliwa sasa

Zab 94: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha