Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 44

44
Kilio cha Kitaifa na Sala kwa ajili ya Msaada
Kwa mwimbishaji. Funzo la Wakorahi.
1Ee Mungu, tumesikia kwa masikio yetu
Baba zetu wametuambia,
Matendo uliyoyatenda siku zao, siku za kale.
2 # Kut 15:17; Kum 7:1; Yos 10:42 Wewe kwa mkono wako uliwafukuza mataifa,
Ukawakalisha wao.
Wewe uliwatesa watu wa nchi,
Ukawaeneza wao.
3 # Yos 24:12; Kum 4:37 Maana si kwa upanga wao walivyoimiliki nchi,
Wala si mkono wao uliowaokoa;
Bali mkono wako wa kuume, naam, mkono wako,
Na nuru ya uso wako, kwa kuwa uliwaridhia.
4 # Zab 74:12 Ee Mungu, Wewe ndiwe mfalme wangu,
Uagize mambo ya wokovu kwa Yakobo.
5 # Dan 8:4 Kwa nguvu zako tutawaangusha watesi wetu;
Kwa jina lako tutawakanyaga watupingao.
6 # Zab 33:16 Maana sitautumainia upinde wangu,
Wala upanga wangu hautaniokoa.
7Bali Wewe ndiwe uliyetuokoa na watesi wetu;
Na watuchukiao umewaaibisha.
8 # Zab 34:2; Rum 2:17; 1 Kor 1:31 Tumejisifia Mungu mchana kutwa,
Na jina lako tutalishukuru milele.
9Lakini umetutupa, umetufedhehesha,
Wala hutoki na majeshi yetu.
10 # Law 26:17; Kum 28:25 Waturudisha nyuma tukampa mtesi kisogo,
Na watuchukiao wanajipatia mateka.
11 # Kum 4:27; 2 Fal 17:6; Zab 60:1; Yer 32:37; Lk 21:24 Umetutoa kama kondoo tuwe chakula,
Na kututawanya kati ya mataifa.
12 # Isa 52:3,4 Wawauza watu wako bila kupata mali,
Wala hukupata faida kwa thamani yao.
13Umetufanya kuwa lawama kwa jirani zetu,
Mzaha na dhihaka kwao wanaotuzunguka.
14Umetufanya kuwa mithali kwa mataifa,
Sababu ya kutikisa kichwa kwa watu wa nchi.
15Mchana kutwa fedheha yangu i mbele yangu,
Na haya ya uso wangu imenifunika,
16 # Zab 8:2 Kwa sauti ya mwenye kulaumu na kukufuru,
Kwa sababu ya adui na mjilipiza kisasi.
17 # Dan 9:13 Haya yote yametupata, bali hatukukusahau,
Wala hatukulihalifu agano lako.
18Hatukuiacha mioyo yetu irudi nyuma,
Wala hatua zetu hazikuiacha njia yako.
19 # Isa 34:13 Hata utuponde katika kao la mbwa-mwitu,
Na kutufunika kwa uvuli wa mauti.
20Ikiwa tumelisahau jina la Mungu wetu,
Au kumnyoshea mungu mgeni mikono yetu;
21 # Ayu 31:14; Zab 139:1; 1 Sam 16:7; Mhu 12:14; Yn 2:25; Mdo 1:24; Rum 2:16; Ebr 4:12; Ufu 2:23 Je! Mungu hatalichunguza neno hilo?
Maana ndiye azijuaye siri za moyo.
22 # Rum 8:36 Hasha! Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa;
Tunafanywa kondoo waendao kuchinjwa.
23Amka, Bwana, mbona umelala?
Ondoka, usitutupe kabisa.
24Mbona unatuficha uso wako,
Na kusahau kuonewa na kudhulumiwa kwetu?
25Maana nafsi yetu imeinama mavumbini,
Tumbo letu limegandamana na nchi.
26Uondoke, uwe msaada wetu,
Utukomboe kwa ajili ya fadhili zako.

Iliyochaguliwa sasa

Zab 44: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha