Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 37:21-40

Zab 37:21-40 SUV

Asiye haki hukopa wala halipi, Bali mwenye haki hufadhili, hukirimu. Maana waliobarikiwa na yeye watairithi nchi, Nao waliolaaniwa na yeye wataharibiwa. Hatua za mtu zaimarishwa na BWANA, Naye aipenda njia yake. Ajapojikwaa hataanguka chini, BWANA humshika mkono na kumtegemeza. Nalikuwa kijana nami sasa ni mzee, Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa Wala mzao wake akiomba chakula. Mchana kutwa hufadhili na kukopesha, Na mzao wake hubarikiwa. Jiepue na uovu, utende mema, Na kukaa hata milele. Kwa kuwa BWANA hupenda haki, Wala hawaachi watauwa wake. Wao hulindwa milele, Bali mzao wa wasio haki ataharibiwa. Wenye haki watairithi nchi, Nao watakaa humo milele. Kinywa chake mwenye haki hunena hekima, Na ulimi wake husema hukumu. Sheria ya Mungu wake imo moyoni mwake. Hatua zake hazitelezi. Mtu asiye haki humvizia mwenye haki, Na kutafuta jinsi ya kumfisha. BWANA hatamwacha mkononi mwake, Wala hatamlaumu atakapohukumiwa. Wewe umngoje BWANA, Uishike njia yake, Naye atakutukuza uirithi nchi, Wasio haki watakapoharibiwa utawaona. Nimemwona mtu asiye haki mkali sana, Akijieneza kama mwerezi wa Lebanoni. Nikapita na kumbe! Hayuko, Nikamtafuta wala hakuonekana. Umwangalie sana mtu mkamilifu, Umtazame mtu mnyofu, Maana mwisho wake mtu huyo ni amani. Wakosaji wataangamizwa pamoja, Wasio haki mwisho wao wataharibiwa. Na wokovu wa wenye haki una BWANA; Yeye ni ngome yao wakati wa taabu. Naye BWANA huwasaidia na kuwaopoa; Huwaopoa na wasio haki na kuwaokoa; Kwa kuwa wamemtumaini Yeye.

Soma Zab 37

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zab 37:21-40

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha