Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 149

149
Sifa kwa Wema wa Mungu kwa Israeli
1 # Isa 42:10 Haleluya.
Mwimbieni BWANA wimbo mpya,
Sifa zake katika kusanyiko la watauwa.
2 # Ayu 35:10; Zek 9:9 Israeli na amfurahie Yeye aliyemfanya,
Wana wa Sayuni na wamshangilie mfalme wao.
3Na walisifu jina lake kwa kucheza,
Kwa matari na kinubi wamwimbie.
4 # Mit 11:20 Kwa kuwa BWANA awaridhia watu wake,
Huwapamba wenye upole kwa wokovu.
5Watauwa na waushangilie utukufu,
Waimbe kwa sauti kuu vitandani mwao.
6 # Kum 7:1-2; Ebr 4:12; Ufu 1:16 Sifa kuu za Mungu na ziwe vinywani mwao,
Na upanga mkali kuwili mikononi mwao.
7Ili kufanya kisasi juu ya mataifa,
Na adhabu juu ya kabila za watu.
8Wawafunge wafalme wao kwa minyororo,
Na wakuu wao kwa pingu za chuma.
9 # Kum 7:1-2; Ufu 5:13; Rum 16:20; 1 Yoh 5:4 Kuwafanyia hukumu iliyoandikwa;
Hiyo ndiyo heshima ya watauwa wake wote.
Haleluya.

Iliyochaguliwa sasa

Zab 149: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha