Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 120

120
Sala ya Ukombozi
Wimbo wa Kupanda Mlima.#120:1 Zaburi za 120-134 huenda ziliimbwa wakati wa kuhiji au kutoka kilimani Yerusalemu ambamo kulikuwa na lile hekalu.
1Katika shida yangu nalimlilia BWANA
Naye akaniitikia.
2Ee BWANA, uiponye nafsi yangu
Na midomo ya uongo na ulimi wa hila.
3Akupe nini, akuzidishie nini,
Ewe ulimi wenye hila?
4Mishale ya mtu hodari iliyochongoka,
Pamoja na makaa ya mretemu.
5 # Mwa 10:2; 1 Sam 25:1; Yer 49:28 Ole wangu mimi!
Kwa kuwa nimekaa katika Mesheki;
Na kufanya maskani yangu
Katikati ya hema za Kedari.
6Nafsi yangu imekaa siku nyingi,
Pamoja naye aichukiaye amani.
7Mimi ni wa amani;
Bali ninenapo, wao huelekea vita.

Iliyochaguliwa sasa

Zab 120: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha