Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hes 9

9
Pasaka katika Sinai
1 # Kut 12:1-13 Kisha BWANA akanena na Musa katika bara ya Sinai, mwezi wa kwanza wa mwaka wa pili baada ya kutoka kwao katika nchi ya Misri, akamwambia, 2#Kut 12:1; Law 23:5; Kum 16:1,2; Hes 28:16; Ebr 10:1Tena, wana wa Israeli na washike sikukuu ya Pasaka kwa wakati wake ulioagizwa. 3Siku ya kumi na nne ya mwezi huu, wakati wa jioni, mtaishika kwa wakati wake ulioagizwa; kwa amri zake zote, na kama hukumu zake zote zilivyo, ndivyo mtakavyoishika. 4Kisha Musa akawaambia wana wa Israeli kwamba waishike sikukuu hiyo ya Pasaka; 5#Yos 5:10Nao wakaishika Pasaka katika mwezi wa kwanza, siku ya kumi na nne ya mwezi, wakati wa jioni, katika bara ya Sinai vile vile kama hayo yote BWANA aliyomwagiza Musa, ndivyo walivyofanya wana wa Israeli.
6 # Hes 5:2; 6:6,7; Yn 18:28; Kut 18:15; Hes 27:2 Basi walikuwako watu waume kadha wa kadha waliokuwa na unajisi kwa ajili ya maiti wa mtu, hata wasiweze kuishika Pasaka siku hiyo; nao wakaenda mbele ya Musa na Haruni, siku hiyo hao watu wakamwambia, 7#1 Kor 5:7,8Sisi tu hali ya unajisi kwa ajili ya maiti wa mtu; nasi tumezuiwa kwa nini hata tusipate kumtolea BWANA matoleo kwa wakati wake ulioagizwa, kati ya wana wa Israeli? 8#Zab 25:14; 85:8; Yn 7:17; Efe 1:9,18; Ebr 3:5,6Musa akawaambia, Ngojeni hapo; hata nipate sikiza BWANA atakaloagiza juu yenu.
9BWANA akanena na Musa, akamwambia, 10Nena na wana wa Israeli, kuwaambia, Mtu wa kwenu, au wa vizazi vyenu, ye yote atakayekuwa na unajisi kwa ajili ya maiti, au akiwako mbali katika safari, na haya yote, ataishika Pasaka kwa BWANA; 11#2 Nya 30:2,15; Kut 12:8mwezi wa pili, siku ya kumi na nne ya mwezi, wakati wa jioni, wataishika; watamla pamoja na mikate isiyotiwa chachu na mboga za uchungu; 12#Kut 12:10,43,46; Yn 19:36wasisaze kitu chake cho chote hata asubuhi, wala wasimvunje mfupa wake; kama hiyo sheria yote ya Pasaka ilivyo ndivyo watakavyoishika. 13#Mwa 17:14; Kut 12:15; Law 17:4; Ebr 6:6; 12:25; Hes 5:31; Gal 3:10; Ebr 10:26Lakini mtu aliye safi, wala hakuwa katika safari, naye amekosa kuishika Pasaka, mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake; kwa sababu hakumtolea BWANA matoleo kwa wakati wake ulioamriwa, mtu huyo atachukua dhambi yake. 14#Kut 12:49Na kama mgeni akiketi kati yenu ugenini, naye ataka kuishika Pasaka kwa BWANA; kama hiyo sheria ya Pasaka ilivyo, na kama amri yake ilivyo, ndivyo atakavyofanya; mtakuwa na sheria moja, kwa huyo aliye mgeni, na kwa huyo aliyezaliwa katika nchi.
Wingu la Moto
15 # Kut 13:21 Na siku hiyo maskani iliposimamishwa, lile wingu likaifunika maskani, yaani, hema ya kukutania; wakati wa jioni likawa juu ya maskani, mfano wa moto, hata asubuhi. 16#Kut 13:21,22; 40:34; Kum 1:33; Neh 9:12Ndivyo ilivyokuwa sikuzote; lile wingu liliifunika kwa mfano wa moto usiku. 17#Kut 40:36,37; Hes 10:11,33,34; Zab 78:14; 80:1; Isa 49:10; Yn 10:4Na kila lilipoinuliwa lile wingu juu ya ile Hema ndipo wana wa Israeli waliposafiri; na mahali lilipokaa lile wingu, ndipo wana wa Israeli walipopiga kambi yao. 18#1 Kor 10:1Kwa amri ya BWANA Wana wa Israeli walisafiri, na kwa amri ya BWANA walipiga kambi; wakati lile wingu ilipokaa juu ya maskani walikaa katika kambi yao. 19Na lile wingu lilipokawia juu ya maskani siku nyingi, ndipo wana wa Israeli walipolinda malinzi ya BWANA, wala hawakusafiri. 20#Zab 48:14; Mit 3:5,6Na pengine lile wingu lilikaa juu ya maskani siku chache; ndipo kwa amri ya BWANA walikaa katika kambi yao, tena kwa amri ya BWANA walisafiri. 21#Mt 28:20Na pengine lile wingu lilikaa tangu jioni hata asubuhi; na lile wingu lilipoinuliwa asubuhi walisafiri, au kama likikaa usiku na mchana pia, lilipoinuliwa lile wingu, ndipo waliposafiri. 22#Kut 40:36,37; Zab 73:24; 107:7; Isa 63:14Ikiwa lile wingu lilikawia, likikaa juu ya maskani siku mbili, au mwezi, au mwaka, wana wa Israeli walikaa katika kambi yao, wasisafiri; 23#Zab 73:24; 107:7; Isa 63:14bali lilipoinuliwa walisafiri. Kwa amri ya BWANA walipiga kambi yao, na kwa amri ya BWANA walisafiri; wakayalinda malinzi ya BWANA, kwa mkono wa Musa.

Iliyochaguliwa sasa

Hes 9: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha