Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hes 33

33
Vituo vya Safari ya Waisraeli Wakitoka Misri
1Hizi ndizo safari za wana wa Israeli, hapo walipotoka nchi ya Misri kwa jeshi zao chini ya mkono wa Musa na Haruni. 2Musa akaandika jinsi walivyotoka katika safari zao, kwa amri ya BWANA; na hizi ndizo safari zao kama kutoka kwao kulivyokuwa. 3#Mwa 47:11; Kut 1:11; 12:37; 12:2; 13:4; Zab 105:38; Isa 52:12; Kut 14:8Wakasafiri kutoka Ramesesi mwezi wa kwanza, siku ya kumi na tano ya mwezi wa kwanza; siku ya pili baada ya Pasaka, wana wa Israeli wakatoka kwa mkono wa nguvu mbele ya macho ya Wamisri wote, 4#Kut 12:12; 18:11; Isa 19:1; Sef 2:11; Ufu 12:8hapo Wamisri walipokuwa wanazika wazaliwa wa kwanza wao wote, BWANA aliokuwa amewapiga kati yao; BWANA akafanya hukumu juu ya miungu yao nayo.
5 # Kut 12:37 Wana wa Israeli wakasafiri kutoka Ramesesi, wakapanga katika Sukothi. 6#Mwa 33:17; Kut 13:20; Yos 13:27; Zab 60:6Kisha wakasafiri kutoka Sukothi, wakapanga Ethamu, palipo katika mwisho wa nyika. 7#Kut 13:17,18; 14:2,9Wakasafiri kutoka Ethamu, na kurudi nyuma hata Pi-hahirothi palipokabili Baal-sefoni; wakapanga mbele ya Migdoli. 8#Kut 14:22; 15:22Wakasafiri kutoka hapo mbele ya Hahirothi, wakapita katikati ya bahari na kuingia jangwani; kisha wakaenda safari ya siku tatu katika nyika ya Ethamu, wakapanga Mara. 9Wakasafiri kutoka Mara, wakafikilia Elimu; huko Elimu palikuwa na chemchemi za maji kumi na mbili, na mitende sabini; nao wakapanga hapo. 10Wakasafiri kutoka Elimu wakapanga karibu na Bahari ya Shamu. 11#Kut 16:1; 17:1Wakasafiri kutoka Bahari ya Shamu, wakapanga katika nyika ya Sini. 12Wakasafiri kutoka nyika ya Sini, wakapanga Dofka. 13Wakasafiri kutoka Dofka, wakapanga Alushi. 14#Kut 17:1; 19:2Wakasafiri kutoka Alushi, wakapanga Refidimu, ambapo hapakuwa na maji ya watu kunywa. 15#Kut 16:1; 19:1,2Wakasafiri kutoka Refidimu, wakapanga katika nyika ya Sinai. 16#Hes 11:34; Kum 9:22Wakasafiri kutoka nyika ya Sinai, wakapanga Kibroth-hataava. 17Wakasafiri kutoka Kibroth-hataava, wakapanga Haserothi. 18#Hes 12:16; Kum 1:1Wakasafiri kutoka Haserothi, wakapanga Rithma. 19Wakasafiri kutoka Rithma, wakapanga Rimon-peresi. 20#Kum 1:1Wakasafiri kutoka Rimon-peresi, wakapanga Libna. 21Wakasafiri kutoka Libna, wakapanga Risa. 22Wakasafiri kutoka Risa, wakapanga Keheletha. 23Wakasafiri kutoka Keheletha, wakapanga katika mlima wa Sheferi 24Wakasafiri kutoka huo mlima wa Sheferi, wakapanga Harada. 25Wakasafiri kutoka Harada, wakapanga Makelothi. 26Wakasafiri kutoka Makelothi, wakapanga Tahathi. 27Wakasafiri kutoka Tahathi wakapanga Tera. 28Wakasafiri kutoka Tera, wakapanga Mithka. 29Wakasafiri kutoka Mithka, wakapanga Hashmona. 30#Kum 10:6Wakasafiri kutoka Hashmona, wakapanga Moserothi. 31Wakasafiri kutoka Moserothi, wakapanga Bene-yakani. 32#Mwa 36:27; Kum 10:6; 1 Nya 1:42Wakasafiri kutoka Bene-yakani, wakapanga Hor-hagidgadi. 33Wakasafiri kutoka Hor-hagidgadi, wakapanga Yotbatha. 34Wakasafiri kutoka Yotbatha, wakapanga Abrona. 35#Kum 2:8; 1 Fal 9:26; 22:48Wakasafiri kutoka Abrona, wakapanga Esion-geberi. 36#Hes 13:21; 20:1; Kum 32:51; Yos 15:1Wakasafiri kutoka Esion-geberi, wakapanga katika nyika ya Sini (ni Kadeshi). 37#Hes 20:22,23; 21:4; Eze 47:19Wakasafiri kutoka Kadeshi wakapanga katika mlima wa Hori, katika mpaka wa nchi ya Edomu, 38#Hes 20:22-28; Kum 10:6; 32:50Haruni akakwea mlima wa Hori, kwa amri ya BWANA, akafa hapo, katika mwaka wa arobaini baada ya wana wa Israeli kutoka katika nchi ya Misri, mwezi wa tano, siku ya kwanza ya mwezi. 39Naye Haruni alikuwa mtu wa umri wa miaka mia na ishirini na mitatu hapo alipokufa katika mlima wa Hori. 40#Hes 21:1; Amu 1:16Ndipo Mkanaani, mfalme wa Aradi, aliyekaa pande za Negebu katika nchi ya Kanaani akasikia habari za kuja kwao wana wa Israeli. 41Nao wakasafiri kutoka mlima wa Hori, wakapanga Salmona. 42Wakasafiri kutoka Salmona, wakapanga Punoni. 43Wakasafiri kutoka Punoni, wakapanga Obothi. 44Wakasafiri kutoka Obothi, wakapanga Iye-abarimu, katika mpaka wa Moabu. 45#Hes 32:34Wakasafiri kutoka Iye-abarimu, wakapanga Dibon-gadi. 46#Yer 48:22; Eze 6:14Wakasafiri kutoka Dibon-gadi, wakapanga Almon-diblathaimu. 47#Hes 21:20; Kum 32:49Wakasafiri kutoka Almon-diblathaimu, wakapanga katika milima ya Abarimu, kukabili Nebo. 48#Hes 22:1Wakasafiri kutoka hiyo milima ya Abarimu, wakapanga katika nchi tambarare za Moabu, karibu na mto wa Yordani, hapo Yeriko. 49Wakapanga karibu na Yordani, tangu Beth-yeshimothi hata kufikilia Abel-shitimu katika nchi tambarare za Moabu.
Maagizo ya Kuishinda Kanaani
50Kisha BWANA akanena na Musa hapo katika nchi tambarare za Moabu, karibu na Yordani, hapo Yeriko, na kumwambia, 51#Kum 7:1; 9:1; Yos 3:17Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mtakapovuka mto wa Yordani na kuingia nchi ya Kanaani, 52#Kut 23:24; 34:12-17; Kum 7:2-5,25,26; Yos 11:12; 23:7; Amu 2:2ndipo mtakapowafukuza wenyeji wote wa hiyo nchi mbele yenu, nanyi mtayaharibu mawe yao yote yenye kuchorwa sanamu, na kuziharibu sanamu zao zote za kusubu, kuvunja-vunja mahali pao pote palipoinuka; 53#Zab 24:1; Kum 10:14; Ayu 41:11; Dan 4:35nanyi mtaishika hiyo nchi kuimiliki na kuketi humo; kwa kuwa mimi nimewapa ninyi hiyo nchi ili mwimiliki. 54#Hes 26:54-56Nanyi mtairithi nchi kwa kufanya kura, kama jamaa zenu zilivyo; hao walio wengi mtawapa urithi zaidi, na hao waliopunguka utawapa kama kupunguka kwao; mahali po pote kura itakapomwangukia mtu ye yote, mahali hapo ni pake; mtarithi kama kabila za baba zenu zilivyo. 55#Yos 23:13; Zab 106:34; Kut 23:33; Eze 28:24Lakini kama hamtaki kuwafukuza wenyeji wa nchi watoke mbele yenu; ndipo hao ambao mtakaowasaza watakuwa kama sindano machoni mwenu, na kama miiba ubavuni mwenu, nao watawasumbua katika hiyo nchi ambayo mwakaa. 56Kisha itakuwa, kama nilivyoazimia kuwatenda wao, ndivyo nitakavyowatenda ninyi.

Iliyochaguliwa sasa

Hes 33: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha