Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mik 2

2
Maovu ya Jamii Yashutumiwa
1 # Est 3:8,9; Isa 32:7; Zab 7:11-14; 36:4; Hos 7:6; Mwa 31:29 Ole wao wakusudiao mambo maovu, na kutenda mabaya vitandani mwao! Kunapopambazuka asubuhi huyafanya, kwa sababu ya katika uwezo wa mikono yao. 2Nao hutamani mashamba, na kuyashika; na nyumba pia, nao huzichukua; nao humwonea mtu na nyumba yake, naam, mtu na urithi wake. 3#Yer 8:3Basi BWANA asema hivi, Angalia, nakusudia jambo baya juu ya jamaa hii, ambalo hamtazitoa shingo zenu, wala hamtakwenda kwa kiburi; kwa maana ni wakati mbaya. 4Siku hiyo watatunga mithali juu yenu, na kuomboleza kwa maombolezo ya huzuni nyingi, na kusema,
Sisi tumeangamizwa kabisa;
Yeye analibadili fungu la watu wangu;
Jinsi anavyoniondolea hilo!
Awagawia waasi mashamba yetu.
5 # Kum 32:8,9 Kwa hiyo hutakuwa na mtu atakayeitupa kamba kwa kura katika mkutano wa BWANA.
6Msitabiri, ndivyo watabirivyo; wasiyatabiri mambo haya; lawama hazikomi. 7Je! Litasemwa neno hili, enyi nyumba ya Yakobo, Roho ya BWANA imepunguzwa? Je! Haya ni matendo yake? Je! Maneno yangu hayamfai yeye aendaye kwa unyofu? 8Lakini siku hizi mmeinuka kama adui za watu wangu; mwaipokonya joho iliyo juu ya nguo za hao wapitao salama kama watu wasiopenda vita. 9Wanawake wa watu wangu mwawatupa nje ya nyumba zao nzuri; watoto wao wachanga mwawanyang’anya utukufu wangu milele. 10#Kum 12:9Ondokeni, mwende zenu; maana hapa sipo mahali pa raha yenu; kwa sababu ya uchafu mtaangamizwa, naam, kwa maangamizo mazito sana. 11Mtu akienda kwa roho ya uongo, akinena maneno ya uongo, akisema, Nitakutabiria habari ya mvinyo na kileo; mtu huyu atakuwa nabii wao watu hawa.
Ahadi kwa Mabaki wa Israeli
12 # Isa 11:11; Mik 4:6,7; Sef 3:19 Hakika nitakukusanya, Ee Yakobo, nyote pia;
Bila shaka nitawakusanya waliobaki wa Israeli;
Nitawaweka pamoja kama kondoo wa Bozra;
Kama kundi la kondoo kati ya malisho yao;
Watafanya mvumo kwa wingi wa watu;
13Avunjaye amekwea juu mbele yao;
Wamebomoa mahali, wakapita mpaka langoni,
Wakatoka nje huko;
Mfalme wao naye amepita akiwatangulia,
Naye BWANA ametangulia mbele yao.

Iliyochaguliwa sasa

Mik 2: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha