Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Law UTANGULIZI

UTANGULIZI
Mambo ya Walawi ndicho kitabu cha tatu katika mfuatano wa vitabu vya Biblia. Hata hivyo kitabu hiki hakizungumzii sana masuala ya Walawi, bali kinaeleza taratibu za kuishi kidini pamoja na kazi za makuhani. Jina “Mambo ya Walawi” linatumiwa kwa kuwa makuhani wote ni Walawi nao ndio viongozi katika masuala ya ibada na taratibu za maisha kidini.
Jambo la kimsingi katika kitabu hiki ni utakatifu wa Mungu na uhusiano kati ya Mungu na mtu aidha mtu na jirani yake. Viumbe vyote na vitu vilivyotengenezwa na mtu vimesongwa na uchafu na kamwe haviwezi kumkaribia Mungu Mtakatifu (16:6). Ili viweze kukubalika na kumkaribia Mtakatifu havina budi kutakaswa na kufanywa vitakatifu kwa kufuata taratibu za ibada ikubalikayo mbele za Mungu (20:26).
Kitabu hiki kinatoa misingi ya sadaka, toba, ondoleo la dhambi, utakaso na upatanisho. Vile vile kina kanuni zinazohusu usafi wa mwili, ndoa, unyumba na chakula. Mungu ni mwaminifu kwa ahadi yake atabariki watiifu na kuhukumu waasi (Sura 26 na 27).
Yaliyomo:
1. Sheria kuhusu sadaka na maongozi ya makuhani, Sura 1–7
2. Huduma katika hema takatifu, Sura 8–10
3. Sheria kuhusu unajisi na utakaso, Sura 11–15
4. Siku ya upatanisho, Sura 16
5. Sheria kuhusu utakatifu, Sura 17–25
6. Baraka na laana, Sura 26
7. Sheria kuhusu nadhiri, Sura 27

Iliyochaguliwa sasa

Law UTANGULIZI: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia