Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yos 19

19
Nchi ya Simeoni
1 # Mwa 49:7 Kisha kura ya pili ilitokea kwa ajili ya Simeoni, maana, kwa ajili ya hiyo kabila ya wana wa Simeoni, kwa kuandama jamaa zao; na urithi wao ulikuwa katikati ya urithi wa wana wa Yuda. 2#1 Nya 4:28-33; Mwa 21:14,31; 26:33; Yos 15:28; Neh 11:26Miji waliyokuwa nayo katika urithi wao ni Beer-sheba, na Sheba, na Molada; 3na Hasarshuali, na Bala, na Esemu; 4#1 Nya 4:29,30na Eltoladi, na Bethuli, na Horma; 5na Siklagi, na Bethmarkabothi, na Hasarsusa; 6na Bethlebaothi, na Sharuheni; miji kumi na mitatu, pamoja na vijiji vyake; 7na Aini, na Rimoni, na Etheri, na Ashani; miji minne, pamoja na vijiji vyake; 8tena vijiji vyote vilivyozunguka miji hiyo kote kote mpaka Baalath-beeri, Rama wa Kusini. Huo ndio urithi wa kabila ya wana wa Simeoni kwa kuandama jamaa zao. 9Huo urithi wa hao wana wa Simeoni ulitoka katika fungu la wana wa Yuda; kwa maana hilo fungu la wana wa Yuda lilikuwa ni kubwa mno kwao; kwa hiyo wana wa Simeoni walikuwa na urithi katikati ya urithi wao.
Nchi za Zabuloni
10Kisha kura ya tatu ilitokea kwa ajili ya wana wa Zabuloni kwa kuandama jamaa zao; na mpaka wa urithi wao ulifikilia hata Saridi; 11#Mwa 49:13; Kut 23:31; Hes 34:6,7; Yos 12:22; 1 Fal 4:12; 1 Nya 6:68kisha mpaka wao ukakwea kwendelea upande wa magharibi, hata kufikilia Marala, nao ukafikilia hata Dabeshethi; nao ukafikilia kijito cha maji kilicho mkabala wa Yokneamu; 12kisha ukazunguka kutoka Saridi kwendelea upande wa mashariki kwa kuelekea maawio ya jua hata kufikilia mpaka wa Kisiloth-ubori; kisha ukatokea hata Daberathi, kisha ukakwea kwendelea Yafia; 13kutoka hapo ukaendelea kuelekea mashariki mpaka Gath-heferi, hata kufikilia Ethkasini; kisha ukatokea huko Rimoni ufikiliao hata Nea; 14kisha mpaka uliizunguka nchi hiyo kwa upande wa kaskazini hata Hanathoni; kisha matokeo yake yalikuwa katika bonde la Iftaeli; 15#Yos 21:34; Amu 1:30; Yos 11:1; 12:20na Katathi, na Nahalali, na Shimroni, na Idala, na Bethlehemu; miji kumi na miwili, pamoja na vijiji vyake. 16#Mdo 17:26Huu ndio urithi wa wana wa Zabuloni kwa kuandama jamaa zao; miji hii pamoja na vijiji vyake.
Nchi ya Isakari
17Kisha kura ya nne ilitokea kwa ajili ya Isakari, maana, ni kwa ajili ya wana wa Isakari kwa kuandama jamaa zao. 18#Yos 15:16; Amu 6:33; 1 Fal 21:1,23; 2 Fal 8:29; 9:15,30; Hos 1:4,5; 1 Sam 28:4; 2 Fal 4:8Na mpaka wao ulifikilia Yezreeli, na Kesulothi, na Shunemu; 19na Hafaraimu, na Shioni, na Anaharathi; 20na Rabithu, na Kishioni, na Ebesi; 21#Yos 21:29na Remethi, na Enganimu, na Enhada, na Bethpasesi; 22#Amu 4:6; 1 Sam 10:3; 1 Nya 6:77; Zab 89:12; Yer 46:18na mpaka ukafikilia hata Tabori, na Shahasuma na Bethshemeshi; na matokeo ya mpaka wao yalikuwa katika mto wa Yordani; miji kumi na sita, pamoja na vijiji vyake. 23Huu ndio urithi wa kabila ya wana wa Isakari kwa kuandama jamaa zao; miji hiyo pamoja na vijiji vyake.
Nchi ya Asheri
24Kisha kura ya tano ilitokea kwa ajili ya kabila ya wana wa Asheri kwa kuandama jamaa zao. 25#2 Sam 2:16; 1 Nya 6:75Na mpaka wao ulikuwa ni Helkathi, na Hali, na Beteni, na Akishafu; 26#1 Fal 18:19; 2 Fal 2:25; 4:25; Isa 35:2; Yer 46:18; Amo 1:2; 9:3; Mik 7:14na Alameleki, na Amadi, na Mishali; nao ukafikilia hata Karmeli upande wa magharibi, tena ulifikilia hata Shihor-libnathi; 27#1 Fal 9:13kisha ukazunguka kuelekea maawio ya jua mpaka Beth-dagoni, nao ukafikilia hata Zabuloni, tena mpaka bonde la Iftaeli upande wa kaskazini hata Bethemeki na Neyeli; kisha ukatokea hata Kabuli upande wa kushoto; 28#Yn 2:1; Mwa 10:15,19; Yos 11:8; Amu 1:31; 10:12; Mdo 27:3na Ebroni, na Rehobu, na Hamoni, na Kana, hata kufikilia Sidoni mkuu; 29#2 Sam 5:11; Mwa 38:5; Amu 1:31; Mik 1:14kisha mpaka ulizunguka kuelekea Rama, na mji wa Tiro ulio na boma; kisha mpaka ulizunguka kuelekea Hosa; na matokeo yake yalikuwa baharini katika nchi ya Akzibu; 30na Uma pia, na Afeka, na Rehobu; miji ishirini na miwili, pamoja na vijiji vyake. 31Huu ndio urithi wa kabila ya wana wa Asheri kwa kuandama jamaa zao; miji hii pamoja na vijiji vyake.
Nchi ya Naftali
32Kisha kura ya sita ikatokea kwa ajili ya wana wa Naftali, maana, ni kwa ajili ya wana wa Naftali kwa kuandama jamaa zao. 33Na mpaka wao ulikuwa kutoka Helefu, tokea ule mwaloni ulio katika Saananimu, na Adami-nekebu, na Yabineeli, hata kufikilia Lakumu; na matokeo yake yalikuwa katika mto wa Yordani; 34#Kum 33:23tena mpaka ulizunguka kwendelea upande wa magharibi hata Aznoth-tabori, tena kutoka hapo ukaendelea mpaka Hukoki; kisha ukafikilia hata Zabuloni upande wa kusini, tena ulifikilia hata Asheri upande wa magharibi, tena ulifikilia hata Yuda hapo katika mto wa Yordani kwa upande wa kuelekea maawio ya jua. 35#Mwa 10:18; Hes 13:21; 1 Fal 8:65; 2 Fal 14:25; Yer 39:5; Kum 3:17; Yos 11:2; 12:3; Mk 6:53; Lk 5:1Na miji yenye boma ilikuwa ni hii, Sidimu, na Seri, na Hamathi, na Rakathi, na Kinerethi; 36na Adama, na Rama, na Hazori; 37na Kedeshi, na Edrei, na Enhasori; 38na Ironi, na Migdal-eli, na Horemu, na Bethanathi, na Bethshemeshi; miji kumi na kenda, pamoja na vijiji vyake. 39Huu ndio urithi wa kabila ya wana wa Naftali kwa kuandama jamaa zao; miji hiyo pamoja na vijiji vyake.
Nchi ya Dani
40Kisha kura ya saba ilitokea kwa ajili ya kabila ya wana wa Dani kwa kuandama jamaa zao. 41#Amu 13:2Na mpaka wa urithi wao ulikuwa ni Sora, na Eshtaoli, na Irishemeshi; 42#Amu 1:35; 1 Fal 4:9na Shaalabini, na Aiyaloni, na Ithla; 43na Eloni, na Timna, na Ekroni; 44na Elteka, na Gibethoni, na Baalathi; 45na Yehudi, na Bene-beraki, na Gathrimoni; 46na Meyarkoni, na Rakoni, pamoja na huo mpaka uliokuwa mkabala wa Yafa. 47#Amu 18:27-29; 18:1; Mwa 49:17Kisha mpaka wa wana wa Dani ulitokea kuwapita wao; kwa kuwa hao wana wa Dani wakakwea na kupigana na Leshemu, na kuutwaa, na kuupiga kwa makali ya upanga, na kuumiliki, nao wakakaa humo, wakauita Dani, kwa kuliandama jina la huyo Dani mzee wao. 48#Hes 26:54; Mdo 17:26Huu ndio urithi wa kabila ya wana wa Dani kwa kuandama jamaa zao; miji hii pamoja na vijiji vyake.
Nchi ya Yoshua
49Basi wakamaliza hiyo kazi yao ya kuigawanya nchi iwe urithi kwa kuandama mipaka yake; kisha wana wa Israeli wakampa Yoshua, mwana wa Nuni, urithi katikati yao; 50#Yos 24:30; 1 Nya 7:24sawasawa na ile amri ya BWANA wakampa mji alioutaka, maana, ni Timnath-sera katika nchi ya vilima ya Efraimu; naye akaujenga huo mji na kukaa mumo.
51 # Hes 34:17; Yos 14:1; 18:1,10; Amu 21:19; Zab 78:58; Yer 7:12; 26:6 Hizi ndizo nchi, ambazo Eleazari kuhani, na Yoshua huyo mwana wa Nuni, pamoja na hao vichwa vya nyumba za mababa ya kabila za wana wa Israeli, walizigawanya kwa njia ya kupiga kura, ziwe urithi, huko Shilo mbele ya BWANA, hapo mlangoni mwa hema ya kukutania. Basi hivyo wakamaliza kazi ya kuigawanya hiyo nchi.

Iliyochaguliwa sasa

Yos 19: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha