Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yon UTANGULIZI

UTANGULIZI
Kitabu hiki ni tofauti na vitabu vingine vya manabii. Ni masimulizi kuhusu Yona, mkazi wa Gath-heferi mji wa Zabuloni, ufalme wa kaskazini uitwao Israeli (2 Fal 14:23, 25). Maana ya jina Yona ni “njiwa”.
Mungu alimtuma nabii Yona kwenda kuwaonya wakazi wa Ninawi, mji wa makao makuu ya taifa la Ashuru. Ili kwamba watubu makosa yao ama sivyo hukumu ya kubomolewa mji wao inawajia. Yona hakuwa tayari kutekeleza wito huo. Bali alijaribu kukimbilia mji mwingine wa mbali Tarshishi ulioko pwani ya Bahari ya Kati.
Wakati huo Israeli ilikuwa imetengemaa kisiasa na kiuchumi, lakini iliogopa sana Ashuru maana ni taifa kubwa, jirani na lililoinuka likiwa na nguvu kijeshi. Pia Ashuru halikuwa na uhusiano mwema na Israeli. Kwa hiyo Yona aliona kuwa sio vema kuwaepushia hukumu ya Mungu bali ilikuwa inawafaa hao ambao aliwahesabu kuwa ni adui na watishia uhuru wa Israeli. Yona alidhani kuwa hukumu ya Mungu kwa Ninawi ingeleta nafuu kwa Waisraeli (3:4-5,10). Yona aliporudishwa akahubiri, Waninawi wakatubu, hakupendezwa.
Mungu alimfundisha Yona kuwa mapenzi yake hayazuiliwi wala hayashindwi, mwanadamu anapaswa kutii. Kwa kuwa Mungu sio Mungu wa Waisraeli tu bali ni wa watu wote na mtawala wa mataifa yote; Binadamu hawezi kumwekea Mungu mipaka ya upendo wake. Mungu hafurahii kuangamia kwa watu aliowaumba, ana upendo na huruma kwa watu wote. Pia anataka watu wote watubu na kusamehewa. Vivyo hivyo watu wake Mungu wanapaswa kuwa na upendo na huruma kwa watu wengine.
Yaliyomo:
1. Yona aasi Mungu, Sura 1
2. Zaburi ya kumshukuru Mungu, Sura 2
3. Toba ya watu wa Ninawi, Sura 3
4. Mungu hapendi watu waangamie, Sura 4

Iliyochaguliwa sasa

Yon UTANGULIZI: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha