Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ayu 41

41
1 # Zab 74:14; 104:26; Isa 27:1 Je! Waweza wewe kumvua mamba kwa ndoana?
Au, kuufunga ulimi wake kwa kamba?
2 # Zab 32:9; Eze 29:4; Isa 30:28; 37:29 Je! Waweza kutia kamba puani mwake?
Au kutoboa taya yake kwa kulabu?
3Je! Atakusihi sana?
Au, atakuambia maneno ya upole?
4Je! Atafanya agano pamoja nawe,
Umtwae kuwa mtumishi wako milele?
5Je! Utamchezea kama ndege?
Au, kumfunga kwa ajili ya wasichana wako?
6Je! Vikosi vya wavuvi watamfanyia biashara?
Watamgawanya kati ya wafanyao biashara?
7Je! Waweza kuijaza ngozi yake na vyuma vyenye ncha,
Au kichwa chake kwa vyusa?
8Mwekee mkono wako;
Vikumbuke vile vita, wala usifanye tena.
9Tazama, kumtamani ni bure;
Je! Hatambwaga chini huyo atakayemtazama?
10 # Ayu 9:4; 40:9-14; 1 Kor 10:22 Hapana aliye mkali hata akathubutu kumwamsha;
Bali ni nani awezaye kusimama mbele yangu mimi?
11 # Ayu 35:7; Rum 11:35; Mwa 14:19; Kum 10:14; Kut 9:29; 19:5; Zab 24:1; 1 Kor 10:26 Ni nani aliyetangulia kunipa hata nimlipe?
Kila kilicho chini ya mbingu nzima ni changu.
12Sitanyamaa kusema habari za via vyake,
Wala nguvu zake kuu, wala umbo lake zuri.
13Ni nani awezaye kumbambua magamba yake?
Ni nani atakayepenya dirii yake maradufu?
14Ni nani awezaye kuifungua milango ya uso wake?
Meno yake yatisha kandokando yake.
15Magamba yake yenye nguvu ndiyo fahari yake,
Yamefungamana pamoja kama kwa kufungwa kwa muhuri.
16Jinsi yalivyoshikamana
Hata upepo hauwezi kupita kati.
17Yamefungamana pamoja;
Yameshikamana, hata hayawezekani kutengwa.
18Kwa kuchemua kwake mwanga humemetuka,
Na macho yake yanafanana na makope ya alfajiri.
19Mienge iwakayo hutoka kinywani mwake,
Na macheche ya moto huruka nje.
20Moshi hutoka katika mianzi ya pua yake,
Kama nyungu ikitokota, na manyasi yawakayo.
21Pumzi zake huwasha makaa,
Na miali ya moto hutoka kinywani mwake.
22Katika shingo yake hukaa nguvu,
Na utisho hucheza mbele yake.
23Manofu ya nyama yake hushikamana;
Yanakazana juu yake; hayawezi kuondolewa.
24Moyo wake una imara kama jiwe;
Naam, imara kama jiwe la chini la kusagia.
25Anapojiinua, mashujaa huogopa;
Kwa sababu ya woga wao huvunjwa moyo.
26Mtu akimpiga kwa upanga, haumwingii;
Wala fumo, wala mshale, wala mkuki wenye ncha.
27Yeye huona chuma kuwa kama nyasi,
Na shaba kama mti uliooza.
28Mshale hauwezi kumkimbiza;
Na mawe ya teo kwake hugeuka kuwa kama makapi.
29Marungu huhesabiwa kama mabua;
Naye hucheka mshindo wa mkuki ukitupwa.
30Pande zake za chini ni kama vigae vikali;
Hutandika malazi kama kuweka chombo cha kupuria nafaka juu ya matope.
31Yeye huchemsha kilindi mfano wa nyungu;
Hufanya bahari kuwa kama mafuta.
32Hufanya mapito yake kung’aa nyuma yake
Hata mtu angedhani kilindi kina mvi.
33Juu ya nchi hapana aliyefanana naye,
Aliyeumbwa pasipo oga.
34Yeye hutazama kila kitu kilicho juu;
Ni mfalme juu ya wote wenye kiburi.

Iliyochaguliwa sasa

Ayu 41: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha