Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isa 5

5
Wimbo wa Shamba la Mizabibu Lisilozaa Matunda
1 # Mt 21:33; Mk 12:1; Lk 20:9; Zab 80:8 Na nimwimbie mpenzi wangu wimbo wa mpenzi wangu katika habari za shamba lake la mizabibu.
Mpenzi wangu alikuwa na shamba la mizabibu,
Kilimani penye kuzaa sana;
2 # Kum 32:6 Akafanya handaki kulizunguka pande zote,
Akatoa mawe yake,
Akapanda ndani yake mzabibu ulio mzuri,
Akajenga mnara katikati yake,
Akachimba shinikizo ndani yake;
Akatumaini ya kuwa utazaa zabibu,
Nao ukazaa zabibu-mwitu.
3 # Rum 3:4 Na sasa, enyi wenyeji wa Yerusalemu, nanyi watu wa Yuda, amueni, nawasihi, kati ya mimi na shamba langu la mizabibu. 4Je! Ni kazi gani iliyoweza kutendeka ndani ya shamba langu la mizabibu nisiyoitenda? Basi, nilipotumaini ya kuwa litazaa zabibu, mbona lilizaa zabibu-mwitu? 5Haya basi, sasa nitawaambieni nitakalolitenda shamba langu la mizabibu; nitaondoa kitalu chake, nalo litaliwa; nitabomoa ukuta wake, nalo litakanyagwa; 6nami nitaliharibu; wala halitapogolewa wala kulimwa, bali litamea mbigili na miiba; nami nitayaamuru mawingu yasinyeshe mvua juu yake. 7Kwa maana shamba la mizabibu la BWANA wa majeshi ndilo nyumba ya Israeli, na watu wa Yuda ni mche wake wa kupendeza; akatumaini kuona hukumu ya haki, na kumbe! Aliona dhuluma; alitumaini kuona haki, na kumbe! Alisikia kilio.
Udhalimu wa Kijamii Washutumiwa
8 # Mik 2:2 Ole wao waongezao nyumba baada ya nyumba, na kuweka shamba karibu na shamba, hata hapana nafasi tena, nanyi hamna budi kukaa peke yenu kati ya nchi! 9BWANA wa majeshi asema katika masikio yangu, Hakika majumba mengi yatakuwa ukiwa, naam, majumba makubwa, mazuri, yatakuwa hayana watu. 10#Law 27:16Kwa maana shamba la mizabibu la eka kumi litatoa bathi moja tu, na homeri ya mbegu itatoa efa tu.
11 # Mit 23:29,30 Ole wao waamkao asubuhi na mapema, wapate kufuata kileo; wakishinda sana hata usiku wa manane mpaka mvinyo imewaka kama moto ndani yao! 12#Amo 6:5; Ayu 34:27; Hos 4:11Na kinubi, na zeze, na matari, na filimbi, na mvinyo, zote ziko katika karamu zao; lakini hawaiangalii kazi ya BWANA wala kuyafikiri matendo ya mikono yake. 13#Isa 1:3,7; Hos 4:6; Lk 19:44; Rum 1:28; 2 Pet 3:5Kwa sababu hiyo watu wangu wamechukuliwa mateka, kwa kukosa kuwa na maarifa; na watu wao wenye cheo wana njaa, na wengi wao waona kiu sana. 14Kwa hiyo kuzimu kumeongeza tamaa yake, kumefunua kinywa chake bila kiasi; na utukufu wao, na wingi wao, na ghasia yao, naye pia afurahiye miongoni mwao, hushuka na kuingia humo. 15Na mtu mnyonge ainamishwa, na mtu mkubwa amedhilika, na macho yao walioinuka hunyenyekezwa, 16bali BWANA wa majeshi ametukuzwa katika hukumu, na Mungu aliye Mtakatifu ametakaswa katika haki. 17Ndipo wana-kondoo watakapolisha kama katika malisho yao wenyewe, na mahali pao waliowanda, palipoachwa ukiwa, wageni watakula.
18Ole wao wavutao uovu kwa kamba za ubatili, na dhambi kama kwa kamba za gari! 19#Isa 66:5; Yer 17:5; Amo 5:18; 2 Pet 3:3Wasema, Na afanye haraka, aihimize kazi yake, tupate kuiona; na likaribie shauri lake aliye Mtakatifu wa Israeli, tupate kuliona.
20Ole wao wasemao kwamba uovu ni wema, na kwamba wema ni uovu; watiao giza badala ya nuru, na nuru badala ya giza; watiao uchungu badala ya utamu, na utamu badala ya uchungu!
21Ole wao walio wenye hekima katika macho yao wenyewe, na wenye busara katika fikira zao wenyewe!
22Ole wao walio hodari kunywa kileo chenye nguvu, watu waume wenye nguvu kuchanganya vileo; 23wampao haki mwenye uovu, ili wapewe ijara, na kumwondolea mwenye haki haki yake!
Uvamizi wa Kigeni Watabiriwa
24 # 2 Fal 17:14; Lk 7:30; Yn 12:48 Kwa hiyo kama vile mwali wa moto uteketezavyo mabua makavu, na kama manyasi makavu yaangukavyo katika mwali wa moto; kadhalika shina lao litakuwa kama ubovu, na ua lao litapeperushwa juu kama mavumbi; kwa sababu wameikataa sheria ya BWANA wa majeshi, na kulidharau neno lake aliye Mtakatifu wa Israeli.
25Kwa sababu hiyo hasira ya BWANA imewaka juu ya watu wake, naye amenyosha mkono wake juu yao; akawapiga, navyo vilima vilitetemeka, na mizoga yao ilikuwa kama takataka katika njia kuu. Pamoja na hayo yote hasira yake haikugeukia mbali, lakini mkono wake umenyoshwa hata sasa.
26Naye atawatwekea bendera mataifa toka mbali,
Naye atawapigia miunzi tokea mwisho wa nchi;
Na tazama, watakuja mbio mbio upesi sana.
27Miongoni mwao hakuna achokaye wala kukwaa;
Hakuna asinziaye wala kulala usingizi;
Wala mshipi wa viuno vyao hautalegea.
Wala ukanda wa viatu vyao hautakatika;
28Mishale yao ni mikali, na pindi zao zote zimepindika;
Kwato za farasi zao zitahesabika kama gumegume;
Na gurudumu zao kama kisulisuli;
29Ngurumo yao itakuwa kama ya simba;
Watanguruma kama wana-simba;
Naam, watanguruma na kukamata mateka,
Na kuyachukua na kwenda zao salama,
Wala hakuna mtu atakayeokoa.
30Nao watanguruma juu yao siku hiyo
Kama ngurumo ya bahari;
Na mtu akiitazama nchi, ataona giza na dhiki
Nayo nuru imetiwa giza katika mawingu yake.

Iliyochaguliwa sasa

Isa 5: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha