Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isa 25

25
Sifa kwa Kukombolewa katika Udhalimu
1 # Kut 15:2; Hes 23:19 Ee BWANA, wewe u Mungu wangu;
Nitakutukuza na kulihimidi jina lako;
Kwa kuwa umetenda mambo ya ajabu,
Mashauri ya kale, kwa uaminifu na kweli.
2 # Yer 51:37 Kwa sababu umefanya mji kuwa ni chungu;
Mji wenye boma kuwa ni magofu;
Jumba la wageni kuwa si mji;
Hautajengwa tena milele.
3 # Ufu 11:13 Kwa hiyo watu walio hodari watakutukuza,
Mji wa mataifa watishao utakuogopa.
4 # Zab 46:1-11; Nah 1:7 Maana umekuwa ngome ya maskini,
Ngome ya mhitaji katika dhiki yake,
Mahali pa kukimbilia wakati wa tufani,
Kivuli wakati wa hari;
Wakati uvumapo upepo wa watu watishao,
Kama dhoruba ipigayo ukuta.
5Kama vile hari katika mahali pakavu
Utaushusha mshindo wa wageni;
Kama ilivyo hari kwa kivuli cha wingu,
Wimbo wa hao watishao utashushwa.
6 # Mit 9:2; Mt 22:4; Dan 7:14; Mt 8:11 Na katika mlima huu BWANA wa majeshi atawafanyia mataifa yote karamu ya vitu vinono, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, karamu ya vinono vilivyojaa mafuta, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, iliyochujwa sana. 7#2 Kor 3:15; Efe 1:17Naye katika mlima huu atauharibu uso wa sitara iliyowekwa juu ya watu wote, na utaji ule uliotandwa juu ya mataifa yote. 8#Isa 26:19; Hos 13:14; 2 Kor 5:4; Ebr 2:14; Mwa 49:18; Tit 2:13; 1 Kor 15:54; Ufu 7:17; 21:4Amemeza mauti hata milele; na Bwana MUNGU atafuta machozi katika nyuso zote; na aibu ya watu wake ataiondoa katika ulimwengu wote; maana BWANA amenena hayo.
9Katika siku hiyo watasema,
Tazama, huyu ndiye Mungu wetu,
Ndiye tuliyemngoja atusaidie;
Huyu ndiye BWANA tuliyemngoja,
Na tushangilie na kuufurahia wokovu wake.
10 # Isa 15:1—16:14; Yer 48:1-47; Eze 25:8-11; Amo 2:1-3; Sef 2:8-11 Kwa maana mkono wa BWANA utatulia katika mlima huu, na Moabu atakanyagwa chini huko aliko, kama vile majani makavu yakanyagwavyo katika maji ya jaa. 11#Ayu 40:11,12; Isa 2:10-12,15-17Naye atanyosha mikono yake katikati yake, kama vile aogeleaye anyoshavyo mikono yake ili aogelee, naye atashusha kiburi chake, pamoja na hila za mikono yake. 12#Isa 26:5Na boma la ngome ya kuta zako ameliinamisha, na kulilaza chini, na kulitupa chini hata mavumbini.

Iliyochaguliwa sasa

Isa 25: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha