Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isa 23

23
Utabiri juu ya Tiro
1 # Yer 25:22; Eze 26:1—28:19; Yoe 3:4-8; Amo 1:9-10; Zek 9:1-4; Mt 11:21-22; Lk 10:13-14 Ufunuo juu ya Tiro. Toeni sauti za uchungu, enyi merikebu za Tarshishi, kwa maana umeharibika kabisa, hata hapana nyumba, hapana mahali pa kuingia; toka nchi ya Kitimu wamefunuliwa habari. 2Tulieni, enyi mkaao kisiwani; wewe ambaye wafanya biashara wa Sidoni, wavukao bahari, walikujaza. 3#Eze 27:3Vitu vilivyopandwa, vya Shihori, mavuno ya Nile, yaliyokuja juu ya maji mengi, ndiyo pato lake, naye alikuwa soko la mataifa. 4Tahayari, Ee Sidoni; kwa maana bahari imenena, hiyo ngome ya bahari ilisema, Sikuona utungu, wala sikuzaa, wala sikulea vijana, wala sikulea wanawali. 5#Isa 19:16Habari itakapofika Misri wataona uchungu sana kwa sababu ya habari ya Tiro. 6Piteni mpaka Tarshishi, enyi mkaao kisiwani, toeni sauti ya uchungu. 7#Isa 22:2Je! Huu ndio mji wenu wa furaha, ambao mwanzo wake ulikuwako tangu siku za kale, ambao miguu yake ilimchukua akae mbali sana? 8#Isa 2:12; Eze 28:2; 1 Tim 3:4Ni nani aliyefanya shauri hili juu ya Tiro, uliotia watu taji, ambao wafanya biashara wake walikuwa wana wa wafalme, na wachuuzi wake ni watu wakuu wa dunia? 9BWANA wa majeshi ndiye aliyefanya shauri hili, ili kuharibu kiburi cha utukufu wote, na kuwaaibisha watu wa duniani wote pia. 10Pita katika nchi yako, kama Nile, Ee binti wa Tarshishi, hapana tena mshipi wa kukuzuia. 11Amenyosha mkono wake juu ya bahari, amezitikisa falme; Bwana ametoa amri katika habari za Kanaani, kuziangamiza ngome zake. 12#Omb 1:6; Hag 2:22; Ufu 18:22Naye akasema, Usizidi kufurahi, ewe bikira uliyeaibishwa, binti wa Sidoni, haya, ondoka, uende hata Kitimu; huko nako hutapata raha. 13#Zab 71:3Tazama, nchi ya Wakaldayo; watu hao hawako tena; Mwashuri ameiweka tayari kwa hayawani wa jangwani; wamesimamisha buruji zao za vita, wameyaharibu majumba yake ya enzi, akaufanya kuwa uharibifu. 14#Isa 2:16; Eze 27:25; Ufu 18:22Pigeni yowe, enyi merikebu za Tarshishi; maana ngome yenu imefanywa ukiwa. 15Basi, itakuwa katika siku ile, Tiro utasahauliwa miaka sabini, kadiri ya siku za mfalme mmoja; hata mwisho wa miaka sabini, Tiro utakuwa kama vile ulivyo wimbo wa kahaba.
16Twaa kinubi, tembea mjini,
Ewe kahaba uliyesahauliwa;
Piga vizuri, imba nyimbo nyingi,
Upate kukumbukwa tena.
17 # Mwa 10:15,19; Yos 11:8; Ufu 17:2 Hata itakuwa mwisho wa miaka sabini, BWANA ataizuru nchi ya Tiro, naye atarudi apate ujira wake, atafanya ukahaba pamoja na falme zote za ulimwengu juu ya uso wa dunia. 18#Kum 28:65,66; Zab 45:12; Omb 1:3; Zek 14:20,21Na biashara yake na ujira wake utakuwa wakfu kwa BWANA, hautawekwa hazinani wala hautawekwa akiba; bali mapato ya biashara yake yatakuwa mali zao wakaao mbele za BWANA, wapate kula na kushiba, na kuvaa mavazi ya fahari.

Iliyochaguliwa sasa

Isa 23: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha