Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Gal 1

1
Salamu
1 # Gal 1:11,12 Paulo, mtume, (si mtume wa wanadamu, wala kutumwa na mwanadamu, bali na Yesu Kristo, na Mungu Baba aliyemfufua kutoka kwa wafu), 2na ndugu wote walio pamoja nami, kwa makanisa ya Galatia; 3#Rum 1:7Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba, na kwa Bwana wetu Yesu Kristo; 4#Gal 2:20; 1 Tim 2:6; Tit 3:14; 1 Yoh 5:19ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili ya dhambi zetu, ili atuokoe na dunia hii mbovu iliyopo sasa, kama alivyopenda Mungu, Baba yetu. 5Utukufu una yeye milele na milele, Amina.
Hakuna Injili Nyingine
6Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, na kugeukia injili ya namna nyingine. 7#Mdo 15:1,24Wala si nyingine; lakini wapo watu wawataabishao na kutaka kuigeuza injili ya Kristo. 8#1 Kor 16:22Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe. 9Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe.
10 # 1 The 2:4 Maana, sasa je! Ni wanadamu ninaowashawishi, au Mungu? Au nataka kuwapendeza wanadamu? Kama ningekuwa hata sasa nawapendeza wanadamu, singekuwa mtumwa wa Kristo.
Paulo Athibitisha Utume wake
11Kwa maana, ndugu zangu, injili hiyo niliyowahubiri, nawajulisha ya kuwa siyo ya namna ya kibinadamu. 12Kwa kuwa sikuipokea kwa mwanadamu wala sikufundishwa na mwanadamu, bali kwa ufunuo wa Yesu Kristo. 13#Mdo 8:3; 22:4-5; 26:9-11Maana mmesikia habari za mwenendo wangu zamani katika dini ya Kiyahudi, kwamba naliliudhi kanisa la Mungu kupita kiasi, nikaliharibu. 14#Mdo 22:3Nami naliendelea katika dini ya Kiyahudi kuliko wengi walio hirimu zangu katika kabila yangu, nikajitahidi sana katika kuyashika mapokeo ya baba zangu. 15#Mdo 9:3-6; 22:6-10; 26:13-18#Rum 1:1; Yer 1:5; Isa 49:1Lakini Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu, akaniita kwa neema yake, 16#Gal 2:7; Mt 16:17alipoona vema kumdhihirisha Mwanawe ndani yangu, ili niwahubiri Mataifa habari zake; mara sikufanya shauri na watu wenye mwili na damu; 17wala sikupanda kwenda Yerusalemu kwa hao waliokuwa mitume kabla yangu; bali nalikwenda zangu Arabuni, kisha nikarudi tena Dameski.
18 # Mdo 9:26-30 Kisha, baada ya miaka mitatu, nalipanda kwenda Yerusalemu ili nionane na Kefa, nikakaa kwake siku kumi na tano. 19#Mt 13:55Lakini sikumwona mtume mwingine, ila Yakobo, ndugu yake Bwana. 20Na hayo ninayowaandikia, angalieni, mbele za Mungu, sisemi uongo. 21#Mdo 9:30Baadaye nalikwenda pande za Shamu na Kilikia. 22Lakini sikujulikana uso wangu na makanisa ya Uyahudi yaliyokuwa katika Kristo; 23ila wamesikia tu ya kwamba huyo aliyetuudhi hapo kwanza, sasa anaihubiri imani ile aliyoiharibu zamani. 24Wakamtukuza Mungu kwa ajili yangu.

Iliyochaguliwa sasa

Gal 1: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha