Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Eze 48

48
Mgawanyo wa Nchi
1 # Hes 34:7-9; Eze 47:15 Basi, haya ndiyo majina ya kabila hizo; toka mwisho wa pande za kaskazini, karibu na njia ya Hethloni, hata maingilio ya Hamathi, hata Hasar-enoni, penye mpaka wa Dameski, yaani, upande wa kaskazini karibu na Hamathi, watakuwa na upande wa mashariki, na upande wa magharibi; Dani fungu moja. 2Tena mpakani mwake Dani, toka upande wa mashariki hata upande wa magharibi; Asheri, fungu moja. 3Na mpakani mwa Asheri, toka upande wa mashariki hata upande wa magharibi; Naftali, fungu moja. 4Na mpakani mwa Naftali, toka upande wa mashariki hata upande wa magharibi; Manase, fungu moja. 5Na mpakani mwa Manase, toka upande wa mashariki hata upande wa magharibi; Efraimu, fungu moja. 6Na mpakani mwa Efraimu, toka upande wa mashariki hata upande wa magharibi; Reubeni, fungu moja. 7Na mpakani mwa Reubeni, toka upande wa mashariki hata upande wa magharibi; Yuda, fungu moja.
8 # Eze 45:1 Na mpakani mwa Yuda, toka upande wa mashariki hata upande wa magharibi, yatakuwapo matoleo mtakayotoa, upana wake mianzi ishirini na tano elfu, na urefu wake sawasawa na moja la mafungu hayo, toka upande wa mashariki hata upande wa magharibi; na mahali patakatifu ni katikati yake. 9Matoleo hayo, mtakayomtolea BWANA, urefu wake ni mianzi ishirini na tano elfu, na upana wake elfu kumi. 10Matoleo hayo matakatifu yatakuwa kwa watu hawa, kwa makuhani; upande wa kaskazini urefu wake ishirini na tano elfu, na upande wa magharibi upana wake elfu kumi, na upande wa mashariki upana wake elfu kumi, na upande wa kusini urefu wake ishirini na tano elfu; na mahali patakatifu pa BWANA patakuwa katikati yake. 11#2 Nya 29:4,5; Neh 9:34; Yer 23:11; Eze 22:26; 44:10; Sef 3:4; Mal 2:7,8Patakuwa kwa makuhani wa wana wa Sadoki, waliotakasika, walioulinda ulinzi wangu, wasioasi, wana wa Israeli walipoasi, kama Walawi walivyoasi. 12Na matoleo hayo ya nchi yatolewayo, yatakuwa kwao kitu kitakatifu sana, karibu na mpaka wa Walawi. 13Na kuukabili mpaka wa makuhani, Walawi watakuwa na fungu, urefu wake ishirini na tano elfu, na upana wake elfu kumi; urefu wote utakuwa ishirini na tano elfu, na upana wake elfu kumi. 14#Kut 22:29; Law 27:10Wala hawatauza sehemu yake, wala kuibadili, wala hawatawapa wengine malimbuko ya nchi; maana ni matakatifu kwa BWANA. 15#Kum 20:5; Eze 42:20; 44:23; 45:6Na mianzi elfu tano iliyosalia katika upana, kuikabili hiyo ishirini na tano elfu, itatumiwa na watu wote, kwa huo mji, na kwa maskani, na kwa viunga, na huo mji utakuwa katikati yake. 16Na vipimo vyake ni hivi; upande wa kaskazini elfu nne na mia tano, na upande wa kusini elfu nne na mia tano, na upande wa mashariki elfu nne na mia tano, na upande wa magharibi elfu nne na mia tano. 17Nao mji utakuwa na malisho; upande wa kaskazini mia mbili na hamsini, na upande wa kusini mia mbili na hamsini, na upande wa mashariki mia mbili na hamsini, na upande wa magharibi mia mbili na hamsini. 18Na mabaki ya urefu wake yaelekeayo matoleo matakatifu, upande wa mashariki yatakuwa elfu kumi, na upande wa magharibi elfu kumi; nayo yatakuwa sawasawa na matoleo matakatifu; na mazao yake yatakuwa ni chakula cha watu wafanyao kazi humo mjini. 19#Ufu 7:5Na hao wafanyao kazi mjini, wa kabila zote za Israeli, watailima nchi hiyo. 20#Hes 24:5; Isa 33:20; Ufu 21:16Matoleo yote yatakuwa ishirini na tano elfu, kwa ishirini na tano elfu; mtatoa matoleo matakatifu, nchi ya mraba, pamoja na milki ya mji.
21 # Yos 18:1; Isa 2:2; 11:10; Hos 1:11; Hag 2:7,9; Mt 11:28; 13:16,17; Yn 12:32; Rum 15:9,12; Ufu 2:1; 21:3 Nayo mabaki yake yatakuwa ya huyo mkuu, upande huu na upande huu wa matoleo matakatifu, na milki ya mji, kuikabili hiyo ishirini na tano elfu ya matoleo, kuelekea mpaka wa mashariki; tena upande wa magharibi kuikabili hiyo ishirini na tano elfu, upande wa kuelekea mpaka wa magharibi; sawa na yale mafungu, hayo yatakuwa ya huyo mkuu; na matoleo matakatifu na mahali patakatifu pa nyumba patakuwa katikati yake. 22Tena tokea milki ya Walawi, na tokea milki ya mji, kwa kuwa ni katikati ya nchi iliyo ya mkuu, katikati ya mpaka wa Yuda na mpaka wa Benyamini, itakuwa ya mkuu.
23Na katika habari za kabila zilizosalia; toka upande wa mashariki hata upande wa magharibi; Benyamini, fungu moja. 24Tena mpakani mwa Benyamini, toka upande wa mashariki hata upande wa magharibi; Simeoni, fungu moja. 25Tena mpakani mwa Simeoni, toka upande wa mashariki hata upande wa magharibi; Isakari, fungu moja. 26Na mpakani mwa Isakari, toka upande wa mashariki hata upande wa magharibi; Zabuloni, fungu moja. 27Na mpakani mwa Zabuloni, toka upande wa mashariki hata upande wa magharibi; Gadi, fungu moja. 28#2 Nya 20:2; Eze 47:19; Mwa 15:18; Hes 34:15; Yos 15:47; Isa 27:12Na mpakani mwa Gadi, upande wa kusini kuelekea kusini, mpaka wake utakuwa toka Tamari, mpaka maji ya Meriba-Kadeshi, mpaka kijito cha Misri, mpaka bahari kubwa. 29#Eze 47:14,21,22Hiyo ndiyo nchi mtakayozigawanyia kabila za Israeli, kuwa urithi wao, na hayo ndiyo mafungu yao, asema Bwana MUNGU.
30 # Ufu 21:12-13 Na matokeo ya mji ndiyo haya; upande wa kaskazini, mianzi elfu nne na mia tano, kwa kupima; 31#Isa 60:18; Ufu 21:12na malango ya mji yatatajwa kwa majina ya kabila za Israeli, malango matatu upande wa kaskazini; lango la Reubeni, moja; lango la Yuda, moja; na lango la Lawi, moja. 32Na upande wa mashariki, elfu nne na mia tano, kwa kupima; na malango matatu; lango la Yusufu, moja; lango la Benyamini, moja; lango la Dani, moja. 33Na upande wa kusini, elfu nne na mia tano kwa kupima; na malango matatu; lango la Simeoni, moja; lango la Isakari, moja; lango la Zabuloni, moja. 34Na upande wa magharibi, elfu nne na mia tano; pamoja na malango yake matatu; lango la Gadi, moja; lango la Asheri, moja; na lango la Naftali, moja. 35#Zab 72:8; Isa 2:2; Mal 1:11; Kut 17:15; Amu 6:24; Ufu 21:3Kuuzunguka ni mianzi kumi na nane elfu; na jina la mji huo tangu siku hiyo litakuwa hili, BWANA yupo hapa.

Iliyochaguliwa sasa

Eze 48: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha