Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kut 21

21
Sheria kuhusu Watumwa
1 # Kut 24:3; Kum 4:14; 6:1 Basi hukumu utakazoziweka mbele ya watu ni hizi 2#Law 25:39-46; Kum 15:12; Yer 34:14Ukimnunua mtumwa wa Kiebrania, atakutumikia muda wa miaka sita; mwaka wa saba atatoka kwako huru bure. 3Kwamba aliingia kwako peke yake tu, atatoka hivyo peke yake; kwamba ameoa, mkewe atatoka aende pamoja naye. 4#Law 25:44Kwamba ni bwana wake aliyempa huyo mke, naye amemzalia wana, wa kiume au wa kike; yule mke na wanawe watakuwa ni mali ya bwana wake, naye mume atatoka peke yake. 5#Kum 15:16Lakini huyo mtumwa akisema waziwazi, Mimi nampenda bwana wangu, na mke wangu na watoto wangu; sitaki mimi kutoka niwe huru; 6#Kut 12:12; 22:8; Kum 16:18; Zab 82:1; 40:6ndipo hapo huyo bwana wake atamleta mbele ya Mungu na kumleta mlangoni, au penye mwimo wa mlango; na bwana wake atalitoboa sikio lake kwa uma; ndipo atamtumikia sikuzote.
7 # Neh 5:5 Mtu akimwuza binti yake awe kijakazi, hatatoka yeye kama watumwa wa kiume watokavyo. 8Kwamba bwana wake hakupendezewa naye, akiwa amemposa, ndipo atakubali akombolewe; hana amri yeye kumwuza aende kwa watu wageni maana amemtenda kwa udanganyifu. 9Kwamba amposa mwanawe, atamtendea kama desturi zipasazo binti zake. 10#1 Kor 7:5Kwamba ajitwalia mke mwingine, chakula chake huyo, na nguo zake, na ngono yake, hatampunguzia. 11Kwamba hamfanyii mambo haya matatu, ndipo atatoka aende bure, pasipo kutolewa mali.
Sheria kuhusu Uhalifu
12 # Law 24:17; Mwa 9:6; Hes 35:30; Mt 26:52 Mtu awaye yote ampigaye mtu, hata akafa, hana budi atauawa huyo. 13#Hes 35:10-34; Kum 19:1-13; Yos 20:1-9; 1 Sam 24:4,10,18Lakini kama hakumvizia, ila Mungu amemtia mkononi mwake; basi nitakuonyesha mahali atakapopakimbilia. 14#Hes 15:30; Kum 19:11; Ebr 10:26; 1 Fal 2:28-34; 2 Fal 11:15Lakini, mtu akimwendea mwenziwe kwa kujikinai, kusudi apate kumwua kwa hila; huyo utamwondoa hata madhabahuni pangu, auawe.
15Ampigaye baba yake au mama yake, sharti atauawa.
16 # Kum 24:7; Mwa 37:28; Kut 22:4 Yeye amwibaye mtu, na kumwuza, au akipatikana mkononi mwake, sharti atauawa huyo
17 # Law 20:9; Mt 15:4; Mk 7:10; Mit 20:20 Yeye amwapizaye baba yake au mama yake, sharti atauawa.
18Watu wakigombana, na mmoja akimpiga mwenziwe kwa jiwe, au kwa konde, asife, lakini yualazwa kitandani mwake; 19#2 Sam 3:29atakapoinuka tena na kuenenda nje kwa kutegemea fimbo, ndipo hapo yule aliyempiga ataachwa; ila atamlipa kwa ajili ya hayo majira yake yaliyompotea, naye atamwuguza hata apone kabisa.
20 # Law 25:43; Efe 6:9 Mtu akimpiga mtumwa wake, au kijakazi chake, kwa fimbo, naye akifa mkononi mwake, hana budi ataadhibiwa. 21#Law 25:45Lakini akipona siku moja au mbili hataadhibiwa; maana, ni mali yake.
22 # Kum 22:18,19 Watu waume wakiteta pamoja, wakamwumiza mwanamke mwenye mimba hata akaharibu mimba, tena yasiwe madhara zaidi; sharti atatozwa mali kama atakavyomwandikia mumewe huyo mwanamke; atalipa kama hao waamuzi watakavyosema. 23Lakini kwamba pana madhara zaidi, ndipo utatoza uhai kwa uhai, 24#Law 24:19-20; Kum 19:21; Mt 5:38; 7:2jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu, 25kuteketeza kwa kuteketeza, jeraha kwa jeraha, chubuko kwa ajili ya chubuko.
26 # Kol 4:1 Mtu akimpiga mtumwa wake jicho, au jicho la kijakazi chake, na kuliharibu; atamwacha huru kwa ajili ya jicho lake. 27Au akimpiga mtumwa wake jino likang’oka, au jino la kijakazi chake, atamwacha huru kwa ajili ya jino lake.
Sheria kuhusu Mali
28 # Mwa 9:5 Ng’ombe akipiga pembe mtu mume au mtu mke, nao wakafa, huyo ng’ombe atauawa kwa kupigwa kwa mawe, nyama yake isiliwe; lakini mwenye huyo ng’ombe ataachiliwa. 29Lakini kwamba huyo ng’ombe alizoea kupiga watu tangu hapo, naye mwenyewe ameonyeshwa jambo hilo, wala asimzuie, naye amemwua mtu mume au mwanamke; huyo ng’ombe atauawa kwa kupigwa kwa mawe, na huyo mwenyewe naye atauawa. 30#Hes 35:31Lakini akiandikiwa ukombozi, ndipo atakapotoa kwa ajili ya uhai wake hicho atakachoandikiwa. 31Akiwa ng’ombe amempiga pembe mtoto wa kiume na kumtumbua, au akiwa amempiga mtoto wa kike, atatendwa kama hukumu hiyo. 32#Zek 11:12,13; Mt 26:15; Flp 2:7Ng’ombe akimtumbua mtumwa mume au kijakazi; mwenye ng’ombe atampa bwana wao shekeli thelathini za fedha, naye ng’ombe atauawa kwa kupigwa kwa mawe.
33Kwamba mtu atafunua shimo, au kuchimba shimo, naye asilifunike, kisha ikawa ng’ombe au punda kutumbukia humo, 34mwenye shimo atalipa; atampa huyo mwenye mnyama fedha, na mnyama aliyekufa atakuwa ni wake.
35Ng’ombe wa mtu akimwumiza ng’ombe wa mtu mwingine hata akafa; ndipo watamwuza huyo ng’ombe aliye hai na kugawanya thamani yake; na ng’ombe aliyekufa pia watamgawanya. 36Au kwamba ilijulikana ya kuwa ng’ombe tangu hapo amezoea kupiga kwa pembe, wala mwenyewe asimzuie; ndipo atakapolipa yeye, ng’ombe kwa ng’ombe, na huyo ng’ombe aliyekufa atakuwa ni wake.

Iliyochaguliwa sasa

Kut 21: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha