Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mhu 6

6
Kukatishwa Tamaa
1Kuna baa nililoliona mimi chini ya jua, nalo linawalemea wanadamu kwa uzito; 2#Kum 8:7-10; Amu 18:10; Ayu 21:10; Zab 17:14; Lk 12:19,20mtu aliyepewa na Mungu mali, ukwasi, na heshima, hata asipungukiwe na kitu cho chote kwa nafsi yake, katika yote anayoyatamani walakini Mungu hamwezeshi kula katika hizo; bali mgeni hula. Hayo ndiyo ubatili hasa, nayo ni ugonjwa mbaya. 3#2 Fal 9:35; Est 7:10; Isa 14:19; Ayu 3:16; Zab 58:8Mtu akizaa watoto mia, akaishi miaka mingi, nazo siku za maisha yake ni nyingi, lakini nafsi yake haikushiba mema; tena ikiwa, zaidi ya hayo, amekosa maziko; mimi nasema, Heri mimba iliyoharibika kuliko huyo; 4yaani, hiyo huja katika ubatili, na huenda gizani, nalo jina lake limefunikwa giza; 5tena, haikuliona jua wala kulifahamu; basi, hii imepata kustarehe kuliko yule; 6naam, ajapoishi miaka elfu mara mbili, asijiburudishe kwa mema; je! Wote hawaendi mahali pamoja?
7 # Mit 16:26; 1 Tim 6:6-8 Kazi yote ya binadamu ni kwa kinywa chake,
Walakini hata hivyo nafsi yake hashibi.
8Kwa maana mwenye hekima hupata faida gani kuliko mpumbavu? Au maskini ana nini kuliko yeye ajuaye kwenda mbele ya walio hai?
9Heri kuona kwa macho,
Kuliko kutanga-tanga kwa tamaa.
Hayo nayo ni ubatili, na kujilisha upepo.
10 # Ayu 9:32; Isa 45:9; Rum 9:19,20 Na awe kitu cho chote, aliitwa jina lake zamani za kale, naye amejulikana kuwa ndiye mwanadamu; wala hawezi kabisa kushindana na yeye aliye na uwezo kuliko yeye mwenyewe. 11Basi, kwa kuwa kuna mambo mengi yaongezayo ubatili, mwanadamu hufaidiwa nini? 12#Yak 4:14; Zab 39:6Kwa maana ni nani ajuaye yaliyo mema ya mwanadamu katika maisha yake, siku zote za maisha yake ya ubatili, anayoishi kama kivuli? Kwa maana ni nani awezaye kumweleza mwanadamu mambo yatakayofuata baada yake chini ya jua?

Iliyochaguliwa sasa

Mhu 6: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha