Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

3 Yoh 1

1
Salamu
1 # Mdo 19:29; Rum 16:23; 1 Kor 1:14; 2 Yoh 1:1 Mzee, kwa Gayo mpenzi, nimpendaye katika kweli.
Gayo Apongezwa kwa Ukarimu wake
2 # 2 Yoh 1:4 Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo. 3Maana nalifurahi mno walipokuja ndugu na kuishuhudia kweli yako, kama uendavyo katika kweli. 4Sina furaha iliyo kuu kuliko hii, kusikia ya kwamba watoto wangu wanakwenda katika kweli.
5Mpenzi, kazi ile ni ya uaminifu uwatendeayo hao ndugu na hao wageni nao, 6#Tit 3:13waliokushuhudia upendo wako mbele ya kanisa; utafanya vizuri ukiwasafirisha kama ipasavyo kwa Mungu. 7#Mdo 20:35; 1 Kor 9:12,15Kwa maana, kwa ajili ya Jina hilo, walitoka, wasipokee kitu kwa Mataifa. 8#Ebr 13:2; 2 Yoh 1:10Basi imetupasa sisi kuwakaribisha watu kama hao, ili tuwe watenda kazi pamoja na kweli.
Diotrefe na Demetrio
9Naliliandikia kanisa neno, lakini Diotrefe, apendaye kuwa wa kwanza kati yao, hatukubali. 10Kwa hiyo, nikija, nitayakumbuka matendo yake atendayo, atoavyo upuzi juu yetu kwa maneno maovu; wala hatoshwi na hayo, ila yeye mwenyewe hawakaribishi hao ndugu, na wale watakao kuwakaribisha, huwazuia, na kuwatoa katika kanisa.
Salamu za Mwisho
11 # 1 Yoh 3:6,9 Mpenzi, usiuige ubaya, bali uige wema. Yeye atendaye mema ni wa Mungu, bali yeye atendaye mabaya hakumwona Mungu. 12#Yn 19:35; 21:24Demetrio ameshuhudiwa na watu wote, tena na ile kweli yenyewe. Nasi pia twashuhudia, nawe wajua ya kwamba ushuhuda wetu ni kweli.
13 # 2 Yoh 1:12 Nalikuwa na mambo mengi ya kukuandikia, lakini sipendi kukuandikia kwa wino na kalamu. 14Lakini nataraji kukuona karibu, nasi tutasema uso kwa uso. 15Amani kwako. Rafiki zetu wakusalimu. Wasalimu hao rafiki zetu, kila mtu kwa jina lake.

Iliyochaguliwa sasa

3 Yoh 1: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha