Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Sam 5

5
Daudi Atiwa Mafuta kuwa Mfalme wa Israeli
1 # 1 Nya 12:23; Mwa 29:14 Ndipo kabila zote za Israeli wakamwendea Daudi huko Hebroni, wakasema naye, wakinena, Tazama, sisi tu mfupa wako na nyama yako. 2#1 Sam 18:13; 16:1; 2 Sam 7:7; Zab 78:71Zamani za kale, hapo Sauli alipokuwa mfalme juu yetu, wewe ndiwe uliyewaongoza Israeli watoke nje, na kuingia ndani. Naye BWANA akakuambia, Wewe utawalisha watu wangu Israeli, nawe utakuwa mkuu juu ya Israeli. 3#1 Nya 11:3; 2 Fal 11:17; Amu 11:11; 1 Sam 23:18Basi wazee wote wa Israeli wakamwendea mfalme huko Hebroni, naye mfalme Daudi akapatana nao huko Hebroni mbele za BWANA; wakamtia Daudi mafuta awe mfalme juu ya Israeli.
4 # 1 Fal 2:11; 1 Nya 3:4; 29:27; 26:31 Daudi alikuwa amepata miaka thelathini alipoanza kutawala, akatawala miaka arobaini. 5Huko Hebroni alitawala miaka saba na miezi sita; na katika Yerusalemu alitawala miaka thelathini na tatu juu ya Israeli wote na Yuda.
Yerusalemu Wafanywa Makao Makuu
6 # Yos 15:63; Amu 1:21; 19:11 Kisha mfalme na watu wake wakaenda Yerusalemu ili kupigana na Wayebusi, wenyeji wa nchi ile; hao ndio waliomwambia Daudi, wakisema, Usipowaondoa vipofu, na viwete, hutaingia humu kamwe; huku wakidhania ya kuwa Daudi hawezi kuingia humo. 7Lakini Daudi aliipiga ngome ya Sayuni; huu ndio mji wa Daudi. 8#1 Nya 11:6Naye Daudi alisema siku hiyo, Yeye atakayewapiga Wayebusi, na apande kwenye mfereji wa maji, na kuwapiga viwete, na hao vipofu, ambao roho yake Daudi inawachukia. Kwa sababu hii watu husema, Wako vipofu na viwete hawawezi kuingia nyumbani. 9#Amu 9:6,20; 1 Fal 9:24; 11:27; 2 Nya 32:5Basi Daudi akakaa ndani ya ngome hiyo, akaiita mji wa Daudi. Kisha Daudi akajenga toka Milo na pande za ndani. 10Naye Daudi akazidi kuwa mkuu; kwa maana BWANA, Mungu wa majeshi, alikuwa pamoja naye.
11 # 1 Fal 5:2; 1 Nya 14:1 Kisha Hiramu, mfalme wa Tiro, akatuma wajumbe kwa Daudi, akampelekea na mierezi, na maseremala, na waashi; nao wakamjengea Daudi nyumba. 12#1 Fal 10:9; 2 Nya 2:11; Est 4:14; Isa 45:4Akajua Daudi ya kwamba BWANA amemweka imara awe mfalme juu ya Israeli, na ufalme wake ameutukuza kwa ajili ya watu wake, Israeli.
13 # Mwa 25:5,6; Kum 17:17 Naye Daudi akazidi kujitwalia masuria na wake huko Yerusalemu baada ya kutoka Hebroni; wakazaliwa zaidi kwa Daudi wana na binti. 14Na haya ndiyo majina ya hao waliozaliwa kwake huko Yerusalemu; Shamua, na Shobabu, na Nathani, na Sulemani, 15na Ibhari, na Elishua; na Nefegi, na Yafia; 16na Elishama, na Eliada, na Elifeleti.
Shambulizi la Wafilisti Lazimwa
17 # 1 Nya 11:16; 2 Sam 23:14 Na hao Wafilisti waliposikia kwamba wamemtia Daudi mafuta ili awe mfalme juu ya Israeli, Wafilisti wote wakapanda kumtafuta Daudi; naye Daudi akapata habari, akashuka akaenda ngomeni. 18#Yos 15:8; Isa 17:5Basi Wafilisti walikuwa wamekuja na kujitawanya bondeni mwa Warefai. 19#Hes 27:21; Yos 9:14; 1 Sam 23:2,4; 2 Sam 2:1Basi Daudi akauliza kwa BWANA, akisema, Je! Nipande juu ya Wafilisti? Utawatia mkononi mwangu? Naye BWANA akamwambia Daudi, Panda; kwa kuwa hakika nitawatia Wafilisti mikononi mwako. 20#Isa 28:21Basi Daudi akaja Baal-perasimu, naye Daudi akawapiga huko; akasema, BWANA amewafurikia adui zangu mbele yangu, kama mafuriko ya maji. Basi akapaita mahali pale Baal-perasimu. 21Nao wakaziacha sanamu zao huko, na Daudi na watu wake wakaziondolea mbali.
22Lakini wakapanda hao Wafilisti tena mara ya pili, wakajitawanya bondeni mwa Warefai. 23Naye Daudi alipouliza kwa BWANA, alisema, Usipande; zunguka nyuma yao, ukawajie huko mbele ya miforsadi. 24Kisha itakuwa, hapo utakapoisikia sauti ya kwenda katika vilele vya miforsadi, ndipo nawe ujitahidi; kwa maana ndipo BWANA ametoka mbele yako awapige jeshi la Wafilisti. 25Ndivyo alivyotenda Daudi, vile vile kama BWANA alivyomwagiza; naye akawapiga Wafilisti toka Geba hata ujapo Gezeri.

Iliyochaguliwa sasa

2 Sam 5: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha