Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Sam 10

10
Kushindwa kwa Waamoni na Washami
1 # 1 Sam 11:1; 2 Sam 17:27; 1 Nya 19:1 Ikawa baadaye, mfalme wa wana wa Amori akafa, akamiliki Hanuni, mwanawe, mahali pake. 2Naye Daudi akasema, Nitamtendea wema Hanuni, mwana wa Nahasi, kama babaye alivyonitendea wema mimi. Basi Daudi akatuma kwa mkono wa watumishi wake, ili kumtuliza kwa habari za babaye. Wakaja watumishi wa Daudi katika nchi ya wana wa Amoni. 3Lakini wakuu wa wana wa Amoni wakamwambia Hanuni, bwana wao, Je! Waona ya kuwa Daudi amemheshimu babayo kwa kutuma kwako wafariji? Je! Daudi hakuwapeleka watumishi wake kwako ili kuuangalia mji, na kuupeleleza, na kuuangamiza? 4#Isa 3:17; 20:4; Yer 13:22,26; Eze 16:37; Mik 1:11; Nah 3:5Basi Hanuni akawatwaa hao watumishi wa Daudi, akawanyoa nusu ya ndevu zao, akawakatia nguo zao katikati, hata matakoni, akawatoa waende zao. 5Watu walipomwambia Daudi habari hizo, akatuma watu kuwalaki; kwa sababu watu hao walikuwa wametahayarika sana. Mfalme akasema, Ngojeni Yeriko, hata mtakapoota ndevu zenu, ndipo mrudi. 6#Mwa 34:30; Kut 5:21; 1 Sam 13:4; 2 Sam 8:3,5Na wana wa Amoni walipoona ya kuwa wamekuwa machukizo kwa Daudi, wana wa Amoni wakatuma na kuwaajiri Washami wa Bethrehobu, na Washami wa Soba, askari ishirini elfu, na mfalme wa Maaka mwenye watu elfu, na watu wa Tobu watu kumi na mbili elfu. 7#2 Sam 23:8Naye Daudi aliposikia akamtuma Yoabu, na jeshi lote la mashujaa. 8Wana wa Amoni wakatoka, wakapanga vita mahali pa kuingilia lango; na Washami wa Soba, na wa Rehobu, na watu wa Tobu, na wa Maaka, walikuwa peke yao uwandani. 9Basi Yoabu alipoona ya kwamba uso wa vita umekuwa juu yake mbele na nyuma, akachagua baadhi ya wateule wote wa Israeli, akawapanga juu ya Washami; 10akawatia nguvu watu waliosalia mkononi mwa Abishai, nduguye, akawapanga juu ya wana wa Amoni. 11Akasema, Wakiwa Washami hodari mno kwangu, ndipo wewe utanisaidia, lakini wana wa Amoni wakiwa ni hodari mno kwako, ndipo mimi nitakuja nikusaidie wewe. 12#Kum 31:6; 2 Nya 19:11; 1 Sam 4:9; 1 Kor 16:13; 1 Sam 3:18; 2 Sam 15:26; 22:31,32; Zab 20:7; 37:3,5,40; Mit 29:25Uwe hodari, tukajitie moyo mkuu, kwa ajili ya watu wetu, na kwa ajili ya miji ya Mungu wetu; naye BWANA afanye yaliyo mema machoni pake. 13Basi Yoabu na watu waliokuwa pamoja naye wakakaribia kupigana na Washami; nao wakakimbia mbele yake. 14Na wana wa Amoni walipoona ya kwamba Washami wamekimbia, wakakimbia nao mbele ya Abishai, wakaingia mjini. Ndipo Yoabu akarudi kutoka kwa wana wa Amoni, akaja Yerusalemu.
15Na Washami walipojiona kuwa wameshindwa mbele ya Israeli, wakakusanyika. 16Naye Hadadezeri akatuma na kuwaleta Washami waliokuwako ng’ambo ya Mto; nao wakaja Helamu, naye Shobaki, jemadari wa jeshi la Hadadezeri, akawaongoza. 17Alipoambiwa Daudi, akakusanya Israeli wote, akavuka Yordani, akaja Helamu. Nao Washami wakajipanga kinyume cha Daudi, wakapigana naye. 18Wakakimbia Washami mbele ya Israeli; naye Daudi akawaua katika Washami, watu wa magari mia saba, na wapanda farasi arobaini elfu, naye akampiga huyo Shobaki, jemadari wa jeshi lao, hata akafa huko. 19#Mwa 14:4Na wafalme wote waliomtumikia Hadadezeri walipojiona kuwa wameshindwa mbele ya Israeli, walifanya amani na Israeli, wakawatumikia. Basi Washami wakaogopa kuwasaidia wana wa Amoni tena.

Iliyochaguliwa sasa

2 Sam 10: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha