Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Nya 7

7
Sulemani Aweka Wakfu Hekalu
1 # 1 Fal 8:54; Isa 65:24; Dan 9:20; Mdo 4:31; 16:25,26; Mwa 15:17; Law 9:23,24; Amu 6:21; 1 Fal 18:38; 1 Nya 21:26; 2 Nya 5:13; Eze 10:3; Ufu 21:23 Basi Sulemani alipokwisha maombi hayo, moto ukashuka kutoka mbinguni, ukateketeza sadaka ya kuteketezwa na dhabihu; utukufu wa BWANA ukaijaza nyumba. 2#2 Nya 5:14Wala makuhani hawakuweza kuingia nyumbani mwa BWANA, kwa kuwa utukufu wa BWANA umeijaza nyumba ya BWANA. 3#2 Nya 5:13; 20:21; Zab 103:17; 136:1Wakatazama wana wa Israeli wote, uliposhuka ule moto, utukufu wa BWANA ulipokuwapo juu ya nyumba; wakasujudu kifulifuli hata nchi sakafuni, wakaabudu, wakamshukuru BWANA, wakisema, Kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele. 4#1 Fal 8:62Ndipo mfalme na watu wote wakatoa dhabihu mbele za BWANA. 5Mfalme Sulemani akatoa sadaka ya ng’ombe ishirini na mbili elfu, na kondoo mia na ishirini elfu. Ndivyo mfalme na watu wote walivyoifanya wakfu nyumba ya Mungu. 6#1 Nya 15:16; 2 Nya 5:12Wakasimama makuhani sawasawa na malinzi yao; Walawi nao pamoja na vinanda vya BWANA, alivyovifanya Daudi mfalme, ili kumshukuru BWANA, kwa maana fadhili zake ni za milele, hapo aliposifu Daudi kwa mikono yao; nao makuhani wakapiga panda mbele yao; nao Israeli wote wakasimama. 7#Hes 16:37; 1 Fal 8:64; 2 Nya 36:14; Ebr 13:10-12Tena Sulemani akaitakasa behewa katikati, iliyokuwa mbele ya nyumba ya BWANA; kwa kuwa hapo ndipo alipotoa sadaka za kuteketezwa, na mafuta ya sadaka za amani; kwa sababu ile madhabahu ya shaba aliyoifanya Sulemani haikutosha kuzipokea sadaka ya kuteketezwa, na sadaka ya unga, na mafuta. 8#1 Fal 8:65; Mwa 15:18; Yos 13:3Basi, wakati ule Sulemani akafanya sikukuu, na Israeli wote pamoja naye, kusanyiko kubwa sana, toka maingilio ya Hamathi mpaka kijito cha Misri, muda wa siku saba. 9Hata siku ya nane wakaita kusanyiko la makini; kwa maana walishika kuitakasa madhabahu siku saba, na sikukuu siku saba. 10#1 Fal 8:66Akawaruhusu watu waende hemani kwao siku ya ishirini na tatu, ya mwezi wa saba, wakifurahi na kuchangamka mioyoni kwa wema wote BWANA aliomfanyia Daudi, na Sulemani, na Israeli watu wake.
11 # 1 Fal 9:1 Hivyo Sulemani akaimaliza nyumba ya BWANA, na nyumba ya mfalme; na yote yaliyomwingia Sulemani moyoni ayafanye nyumbani mwa BWANA, na nyumbani mwake mwenyewe, akayafanikisha.
Bwana Amtokea Sulemani Mara ya Pili
12 # Mwa 12:7; Kum 12:5; Zab 78:68,69; 132:13,14 BWANA akamtokea Sulemani usiku, akamwambia, Nimesikia uliyoyaomba, na mahali hapa nimejichagulia kuwa nyumba ya dhabihu. 13#2 Nya 6:26Nikizifunga mbingu isiwe mvua, tena nikiamuru nzige kula nchi, au nikiwapelekea watu wangu tauni; 14#Yak 4:10; 2 Nya 6:27ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao. 15#2 Nya 6:40Sasa macho yangu yatafumbuka, na masikio yangu yatasikiliza maombi ya watu waombao mahali hapa. 16#2 Nya 6:6Maana sasa nimeichagua nyumba hii na kuitakasa, ili kwamba jina langu lipate kuwako huko milele; yatakuwako na macho yangu, na moyo wangu daima. 17#1 Fal 9:4Nawe, ukienda mbele yangu kama alivyokwenda Daudi baba yako, ufanye sawasawa na yote niliyokuamuru, na kuzishika sheria zangu na hukumu zangu; 18#2 Nya 6:16ndipo nitakithibitisha kiti cha enzi cha ufalme wako, kama nilivyoagana na Daudi baba yako, nikisema, Hutakosa kuwa na mtu wa kutawala katika Israeli.
19 # Law 26:14; Kum 28:15 Lakini mkigeuka, na kuziacha sheria zangu na amri zangu nilizoweka mbele yenu, mkienda, na kuitumikia miungu mingine, na kuiabudu; 20#Zab 5:5ndipo nitawang’oa katika nchi yangu niliyowapa; na nyumba hii niliyoitakasa kwa jina langu, nitaiondosha itoke mbele zangu, nami nitaifanya kuwa mithali na tukano katikati ya watu wote. 21#Yer 7:14; 22:8; Omb 2:15; Kum 29:24Na nyumba hii, iliyo juu, kila apitaye ataona ushangao, atasema, Mbona BWANA ameitendea hivi nchi hii, na nyumba hii? 22#Amu 2:13; 2 Fal 17:18; 2 Nya 36:16; Dan 9:12Nao watajibu, Kwa sababu walimwacha BWANA, Mungu wa baba zao, aliyewaleta kutoka nchi ya Misri, wakashikamana na miungu mingine, wakaiabudu, na kuitumikia; kwa hiyo ameyaleta mabaya haya yote juu yao.

Iliyochaguliwa sasa

2 Nya 7: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha