Zekaria 6:1-8
Zekaria 6:1-8 NENO
Nikatazama juu tena: nikaona mbele yangu magari manne ya vita yakija kutoka kati ya milima miwili, milima ya shaba! Gari la kwanza lilivutwa na farasi wekundu, la pili lilivutwa na farasi weusi, la tatu lilivutwa na farasi weupe, na gari la nne lilivutwa na farasi wa madoadoa ya kijivu, wote wenye nguvu. Nikamuuliza malaika aliyekuwa akizungumza nami, “Hawa ni nani, bwana wangu?” Malaika akanijibu, “Hizi ni roho nne za mbinguni zisimamazo mbele ya uwepo wa Bwana wa dunia yote, zinatoka kwenda kufanya kazi yake. Gari linalovutwa na farasi weusi linaelekea katika nchi ya kaskazini, la farasi weupe linaelekea magharibi, na la farasi wa madoadoa ya kijivu linaelekea kusini.” Hao farasi wenye nguvu walipokuwa wakitoka, walikuwa wakijitahidi kwenda duniani kote. Akasema, “Nenda duniani kote!” Kwa hiyo wakaenda duniani kote. Kisha akaniita, “Tazama, wale wanaoenda kuelekea nchi ya kaskazini wamepumzisha Roho wangu katika nchi ya kaskazini.”