Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Wimbo Utangulizi

Utangulizi
Kitabu hiki kinaitwa “Wimbo Ulio Bora,” yaani “Wimbo Mzuri kupita Nyimbo Zote.” Hii ni tafsiri ya moja kwa moja kutoka maneno ya Kiebrania, “Shir Hash-Shirim,” na kwa Kiyunani “Asma Asmaton.” Hili ndilo chimbuko la jina linalokitambulisha kitabu hiki.
Mwandishi
Sulemani.
Kusudi
Kuthibitisha utakatifu wa Mungu, furaha, heshima na upendo katika ndoa kulingana na kusudi la Mungu, na kudhihirisha upendo wa Mungu kwa watu wake.
Mahali
Bustani ya mwanamke Mshulami na jumba la kifalme.
Tarehe
Inadhaniwa kuwa miaka ya mwanzo ya utawala wa Sulemani.
Wahusika Wakuu
Mfalme Sulemani, Mwanamke Mshulami, na rafiki zao.
Wazo Kuu
Upendo wa dhati kati ya mume na mke katika ndoa.
Mambo Muhimu
Mambo yanayohusu upendo na ndoa.
Yaliyomo
Bibi arusi na bwana arusi (1:1–2:7)
Sifa za mpenzi wake (2:8–3:5)
Kumsifu bibi arusi (3:6–5:1)
Upendo wenye msukosuko (5:2–7:9)
Urafiki ambao haujavunjika (7:10–8:14).

Iliyochaguliwa sasa

Wimbo Utangulizi: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia