Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 76

76
Zaburi 76
Mungu Wa Israeli Ni Mhukumu Wa Dunia Yote
Kwa mwimbishaji. Kwa ala za nyuzi za muziki. Zaburi ya Asafu. Wimbo.
1 Katika Yuda, Mungu anajulikana,
jina lake ni kuu katika Israeli.
2 Hema lake liko Salemu,
makao yake katika Sayuni.
3 Huko alivunja mishale imetametayo,
ngao na panga, silaha za vita.
4 Wewe unangʼaa kwa mwanga,
mwenye fahari zaidi ya milima yenye utajiri wa wanyama pori.
5 Mashujaa hulala wametekwa nyara,
hulala usingizi wao wa mwisho;
hakuna hata mmoja wa watu wa vita
anayeweza kuinua mikono yake.
6 Kwa kukemea kwako, Ee Mungu wa Yakobo,
farasi na gari la vita vilikaa kimya.
7 Wewe peke yako ndiye wa kuogopwa.
Ni nani awezaye kusimama mbele yako unapokasirika?
8 Kutoka mbinguni ulitamka hukumu,
nayo nchi ikaogopa, ikawa kimya:
9 wakati wewe, Ee Mungu, ulipoinuka kuhukumu,
kuwaokoa wote walioonewa katika nchi.
10 Hakika ghadhabu yako dhidi ya wanadamu inakuletea sifa,
na masalia ya ghadhabu yako unajifunga mshipi.
11 Wekeni nadhiri kwa Bwana Mungu wenu na kuzitimiza;
nchi zote za jirani na walete zawadi
kwa Yule astahiliye kuogopwa.
12Huvunja roho za watawala;
anaogopwa na wafalme wa dunia.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 76: NEN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha