Zaburi 24:7-10
Zaburi 24:7-10 NENO
Inueni vichwa vyenu, enyi malango, inukeni enyi milango ya kale, ili mfalme wa utukufu apate kuingia. Ni nani huyu Mfalme wa utukufu? Ni BWANA aliye na nguvu na uweza, ni BWANA aliye hodari katika vita. Inueni vichwa vyenu, enyi malango, viinueni juu enyi milango ya kale, ili Mfalme wa utukufu apate kuingia. Ni nani yeye, huyu Mfalme wa utukufu? Ni BWANA wa majeshi; yeye ndiye Mfalme wa utukufu.