Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 146

146
Zaburi 146
Kumsifu Mungu mwokozi
1Msifuni Bwana!#146:1 Msifuni Bwana kwa Kiebrania ni Hallelu Yah; pia 146:10.
Ee nafsi yangu, umsifu Bwana,
2Nitamsifu Bwana maisha yangu yote;
nitamwimbia Mungu wangu sifa
wakati wote ningali hai.
3Usiweke tumaini lako kwa wakuu,
kwa wanadamu ambao hufa,
ambao hawawezi kuokoa.
4Roho yao itokapo hurudi mavumbini,
siku hiyo hiyo mipango yao yote hukoma.
5Heri yeye ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake,
ambaye tumaini lake ni katika Bwana, Mungu wake,
6Muumba wa mbingu na nchi,
na bahari na vyote vilivyomo:
Bwana anayedumu kuwa mwaminifu
milele na milele.
7Naye huwapatia haki waliodhulumiwa,
na kuwapa wenye njaa chakula.
Bwana huwaweka wafungwa huru,
8 Bwana huwafumbua vipofu macho,
Bwana huwainua waliolemewa na mizigo yao,
Bwana huwapenda wenye haki.
9 Bwana huwalinda wageni
na kuwategemeza yatima na wajane,
lakini hupinga njia za waovu.
10 Bwana atamiliki milele,
Mungu wako, ee Sayuni,
kwa vizazi vyote.
Msifuni Bwana.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 146: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia