Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 141

141
Zaburi 141
Maombi ya kuhifadhiwa dhidi ya uovu
Zaburi ya Daudi.
1Ee Bwana, ninakuita, njoo kwangu hima.
Sikia sauti yangu ninapokuita.
2Maombi yangu na yafike mbele zako kama uvumba;
kuinua mikono yangu juu na kuwe kama dhabihu ya jioni.
3Ee Bwana, weka mlinzi kinywani mwangu,
weka ulinzi mlangoni mwa midomo yangu.
4Usiuache moyo wangu uvutwe katika jambo baya,
nisije nikashiriki katika matendo maovu
pamoja na watu watendao mabaya,
wala nisije nikala vyakula vyao vya anasa.
5Mtu mwenye haki na anipige: ni jambo la huruma;
na anikemee: ni mafuta kichwani mwangu.
Kichwa changu hakitalikataa.
Hata hivyo, maombi yangu daima
ni kinyume cha watenda maovu.
6Watawala wao watatupwa chini
kutoka majabali,
waovu watajifunza kwamba maneno yangu
yalikuwa kweli.
7Watasema, “Kama mtu anavyolima na kuvunja ardhi,
ndivyo mifupa yetu imetawanywa kwenye mlango wa kaburi.”
8Lakini nimekaza macho yangu kwako, Ee Bwana Mwenyezi,
ndani yako nimekimbilia, usiniache nife.
9Niepushe na mitego waliyonitegea,
kutokana na mitego iliyotegwa na watenda maovu.
10Waovu na waanguke kwenye nyavu zao wenyewe,
wakati mimi ninapita salama.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 141: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia