Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 119:25-32

Zaburi 119:25-32 NEN

Nimelazwa chini mavumbini, yahifadhi maisha yangu sawasawa na neno lako. Nilikueleza njia zangu ukanijibu, nifundishe sheria zako. Nijulishe mafundisho ya mausia yako, nami nitatafakari maajabu yako. Nafsi yangu imechakazwa kwa huzuni, uniimarishe sawasawa na neno lako. Niepushe na njia za udanganyifu, kwa neema unifundishe sheria zako. Nimechagua njia ya kweli, nimekaza moyo wangu katika sheria zako. Nimengʼangʼania sheria zako, Ee BWANA, usiniache niaibishwe. Nakimbilia katika njia ya maagizo yako, kwa kuwa umeuweka moyo wangu huru.

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha