Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 119:17-24

Zaburi 119:17-24 NEN

Mtendee mema mtumishi wako, nami nitaishi; nitalitii neno lako. Yafungue macho yangu nipate kuona mambo ya ajabu katika sheria yako. Mimi ni mgeni duniani, usinifiche amri zako. Nafsi yangu inataabika kwa shauku kubwa juu ya sheria zako wakati wote. Unawakemea wenye majivuno, waliolaaniwa waendao mbali na amri zako. Niondolee dharau na dhihaka, kwa kuwa ninazishika sheria zako. Ingawa watawala huketi pamoja na kunisingizia, mtumishi wako atatafakari juu ya maagizo yako. Sheria zako ni furaha yangu, nazo ni washauri wangu.

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha