Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mithali 10:1-10

Mithali 10:1-10 NENO

Mithali za Sulemani: Mwana mwenye hekima huleta furaha kwa baba yake, lakini mwana mpumbavu huleta huzuni kwa mama yake. Hazina zilizopatikana kwa njia mbaya hazifai, lakini uadilifu huokoa kutoka mautini. BWANA hawaachi waadilifu kukaa njaa, lakini hupinga tamaa ya mtu mwovu. Mikono mivivu hufanya mtu kuwa maskini lakini mikono yenye bidii huleta utajiri. Yeye akusanyaye mazao wakati wa kiangazi ni mwana mwenye hekima, lakini yeye alalaye wakati wa mavuno ni mwana mwenye kuaibisha. Baraka huwa taji kichwani mwa mwenye haki, lakini jeuri hufunika kinywa cha mwovu. Kumbukumbu ya mwenye haki itakuwa baraka, lakini jina la mwovu litaoza. Mwenye hekima moyoni hupokea maagizo, lakini mpumbavu apayukaye huangamia. Mtu mwadilifu hutembea salama, lakini mtu aendaye katika njia zilizopotoka atagunduliwa. Yeye akonyezaye kwa nia mbaya husababisha huzuni, naye mpumbavu apayukaye huangamia.