Wafilipi 3:4-6
Wafilipi 3:4-6 NENO
ingawa mimi mwenyewe ninazo sababu za kuutumainia mwili. Kama mtu yeyote akidhani anazo sababu za kuutumainia mwili, mimi zaidi. Nilitahiriwa siku ya nane, mimi ni Mwisraeli wa kabila la Benyamini, Mwebrania wa Waebrania. Kwa habari ya sheria, ni Farisayo, kwa habari ya juhudi, nilikuwa nalitesa kanisa, kuhusu haki inayopatikana kwa sheria, sikuwa na hatia.