Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Filemoni Utangulizi

Utangulizi
Waraka huu mfupi umeainishwa na nyaraka za Waefeso, Wakolosai na Wafilipi kama mojawapo wa nyaraka Paulo alizoandika akiwa gerezani. Aliandikia Filemoni na Afia, mwanamke Mkristo (ambaye huenda alikuwa mkewe Filemoni), na Arkipo, na kanisa lililokuwa likikusanyika nyumbani mwa Filemoni.
Onesimo alikuwa mtumwa aliyetoroka kutoka kwa Filemoni huko Kolosai akaenda Rumi, ambako aliokoka. Onesimo, kama mtumwa, alikuwa mali ya Filemoni kisheria.
Mwandishi
Mtume Paulo.
Kusudi
Kumhimiza Filemoni amsamehe Onesimo, mtumwa aliyemtoroka, na amkubali kama ndugu Mkristo katika imani.
Mahali
Rumi.
Tarehe
Mnamo 60 B.K.
Wahusika Wakuu
Paulo, Filemoni, na Onesimo.
Wazo Kuu
Paulo alimwandikia Filemoni kumshawishi amkubali Onesimo kurudi kwake, na amsamehe aliyomkosea.
Mambo Muhimu
Barua hii ni kielelezo cha ukarimu wa Kikristo. Paulo alishukuru kwa moyo wa ukarimu ambao tayari Filemoni alikuwa ameonesha kwa Wakristo wenzake. Paulo alikuwa na uwezo wa kumwamuru Filemoni, lakini alimwomba Filemoni ampokee Onesimo kwa upendo.
Yaliyomo
Salamu (1‑3)
Shukrani na maombi (4‑7)
Paulo anamtetea Onesimo (8‑22)
Salamu za mwisho (23‑25).

Iliyochaguliwa sasa

Filemoni Utangulizi: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia