Nehemia Utangulizi
Utangulizi
Vitabu vya Ezra na Nehemia vinaenda sambamba na vitabu vya Mambo ya Nyakati, vikisimulia habari zinazofuata matukio ya Mambo ya Nyakati. Kitabu cha Nehemia kimepewa jina la mhusika wake mkuu ambaye ni Nehemia. Katika andiko la Kiebrania, kitabu hiki ni sehemu ya kitabu cha Ezra. Inaaminika kwamba nabii Malaki alikuwa akihudumu katika kipindi hiki.
Mwandishi
Inasadikika kwamba Nehemia au Ezra, au wote wawili waliandika kitabu hiki, kwa sababu mwanzoni Ezra na Nehemia vilikuwa kitabu kimoja.
Kusudi
Habari za kurudi kwa Wayahudi kutoka uhamishoni, na kujengwa kwa ukuta wa Yerusalemu.
Mahali
Yerusalemu.
Tarehe
Pengine mnamo 445–432 K.K.
Wahusika Wakuu
Nehemia, Ezra, Tobia na Sanbalati.
Wazo Kuu
Kitabu hiki kinaonesha kutimizwa kwa unabii wa Zekaria na Danieli kuhusu kujengwa upya kuta za Yerusalemu.
Mambo Muhimu
Kujengwa kwa ukuta wa Yerusalemu, na kurejeshwa kwa utaratibu wa ibada.
Yaliyomo
Nehemia anazijenga kuta za Yerusalemu, watu waliorudi (1:1–7:73)
Marekebisho chini ya Ezra na Nehemia (7:73–13:31).
Iliyochaguliwa sasa
Nehemia Utangulizi: NENO
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Biblia Takatifu™ Neno™
Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Version™
Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 by Biblica, Inc.
Used with permission. All rights reserved worldwide.