Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mathayo 16:13-18

Mathayo 16:13-18 NENO

Basi Yesu alipofika katika eneo la Kaisaria-Filipi, akawauliza wanafunzi wake, “Watu husema kwamba mimi Mwana wa Adamu ni nani?” Wakamjibu, “Baadhi husema ni Yohana Mbatizaji; wengine husema ni Eliya; na bado wengine husema ni Yeremia au mmoja wa manabii.” Akawauliza, “Je, ninyi mnasema mimi ni nani?” Simoni Petro akamjibu, “Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.” Naye Yesu akamwambia, “Heri wewe, Simoni Bar-Yona, kwa maana hili halikufunuliwa kwako na mwanadamu, bali na Baba yangu aliye mbinguni. Nami nakuambia, wewe ndiwe Petro na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu, hata malango ya Kuzimu hayataweza kulishinda.