Mathayo 15:17-19
Mathayo 15:17-19 NENO
Je, hamwelewi kwamba chochote kiingiacho kinywani huenda tumboni, na hatimaye hutolewa nje kikiwa uchafu? Lakini kitokacho kinywani hutoka moyoni, na hiki ndicho kimtiacho mtu unajisi. Kwa maana ndani ya moyo hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati, wizi, ushahidi wa uongo na masingizio.