Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Malaki Utangulizi

Utangulizi
Maana ya jina Malaki ni “Mjumbe Wangu” au “Mjumbe wa Bwana”. Malaki aliishi baada ya Hekalu la pili kujengwa. Maisha ya uchaji wa Mungu ya Wayahudi yalikuwa mabaya: Walikuwa wamekengeuka, wakawaoa wanawake wa mataifa mengine, na wakaacha kutoa zaka na dhabihu kwa Mungu. Habari hizi zinafanana sana na mwisho wa kitabu cha Nehemia, ambaye kuna uwezekano mkubwa aliishi wakati mmoja na Malaki.
Mwandishi
Malaki.
Kusudi
Kuwahimiza watu wafanye mabadiliko thabiti ya kimsingi katika maisha yao kwa kuziacha dhambi zao ili kurejesha uhusiano wao na Mungu, na kuwakumbusha kuhusu upendo wa Mungu.
Mahali
Yerusalemu na Hekaluni.
Tarehe
Mnamo 430 K.K.
Wahusika Wakuu
Malaki, makuhani, na watu wa Yuda.
Wazo Kuu
Upendo wa Mungu hauna kikomo wala mipaka.
Mambo Muhimu
Kitabu hiki kinaonesha kuwa Hekalu lilijengwa tena, na dhabihu na sikukuu zikarudishwa. Ufahamu wa jumla wa Sheria ulirudishwa tena na Ezra, na kurudi kwao nyuma kimaadili kulikofuatia kulitokea zaidi miongoni mwa makuhani.
Yaliyomo
Upendo wa Mungu kwa Israeli (1:1‑5)
Israeli wamtukana Mungu (1:6–2:16)
Hukumu ya Mungu na ahadi yake (2:17–4:6).

Iliyochaguliwa sasa

Malaki Utangulizi: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia