Luka 5:12-13
Luka 5:12-13 NENO
Ikawa siku moja Yesu alipokuwa katika mji fulani, mtu mmoja mwenye ukoma mwili mzima akamjia. Alipomwona Yesu, alianguka chini hadi uso wake ukagusa ardhi, akamsihi akisema, “Bwana, ukitaka, unaweza kunitakasa.” Yesu akanyoosha mkono wake, akamgusa yule mtu, akamwambia, “Nataka. Takasika!” Na mara ukoma wake ukatakasika.