Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Luka 22:63-71

Luka 22:63-71 NENO

Watu waliokuwa wanamlinda Yesu wakaanza kumdhihaki na kumpiga. Wakamfunga kitambaa machoni na kumuuliza, “Tabiri! Tuambie ni nani aliyekupiga?” Wakaendelea kumtukana kwa matusi mengi. Kulipopambazuka, Baraza la Wazee, yaani viongozi wa makuhani na walimu wa sheria, wakakutana pamoja, naye Yesu akaletwa mbele yao. Wakamwambia, “Kama wewe ndiwe Kristo, tuambie.” Yesu akawajibu, “Hata nikiwaambia, hamtaamini. Nami nikiwauliza swali, hamtanijibu. Lakini kuanzia sasa, Mwana wa Adamu ataketi mkono wa kuume wa Mungu Mwenye Nguvu.” Wote wakauliza, “Wewe basi ndiwe Mwana wa Mungu?” Yeye akawajibu, “Ninyi mwasema kwamba mimi ndiye.” Kisha wakasema, “Tuna haja gani tena ya ushahidi zaidi? Tumesikia wenyewe kutoka kinywani mwake.”