Yona Utangulizi
Utangulizi
Jina Yona maana yake ni “Hua”. Kitabu hiki kinaelezea yale yaliyomtokea Yona kama mjumbe wa Mungu. Yona alikuwa ameagizwa na Mungu aende kuwaonya watu wa Ninawi juu ya hukumu iliyokuwa inakuja. Alijaribu kumkimbia Mungu na kuelekea Tarshishi, upande wa magharibi wa Israeli badala ya kuelekea Ninawi iliyokuwa kaskazini mashariki. Yona alitupwa baharini akamezwa na samaki mkubwa sana ambaye alimtapika pwani ya mashariki mwa Bahari ya Kati (Mediterania). Hatimaye alikwenda Ninawi na kuwaonya watu kuhusu hukumu ya Mungu na watu wa Ninawi walitubu. Badala ya kufurahia jambo hili, Yona alihuzunika na kuvunjika moyo kwa sababu Mungu alionesha rehema na kughairi hukumu dhidi ya watu wa Ninawi.
Mwandishi
Yona mwana wa Amitai.
Kusudi
Kuonesha ukuu wa rehema za Mungu na wokovu kwa mwanadamu. Pia, kuonesha jinsi ambavyo mwanadamu hawezi kukimbia wito wa Mungu.
Mahali
Inaweza kuwa Israeli au Ninawi.
Tarehe
Inadhaniwa kuwa mnamo 785–760 K.K.
Wahusika Wakuu
Yona, nahodha wa meli na mabaharia, mfalme wa Ninawi, na Waninawi wote.
Wazo Kuu
Ukuu wa rehema za Mungu.
Mambo Muhimu
Rehema za Mungu na upendo wa Mungu kwa watu wote.
Yaliyomo
Yona amkimbia Mungu (1:1‑17)
Maombi ya Yona na kuokolewa (2:1‑10).
Yona aenda Ninawi (3:1‑10)
Hasira ya Yona kwa ajili ya huruma ya Bwana (4:1‑11).
Iliyochaguliwa sasa
Yona Utangulizi: NENO
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Biblia Takatifu™ Neno™
Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Version™
Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 by Biblica, Inc.
Used with permission. All rights reserved worldwide.