Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yoeli Utangulizi

Utangulizi
Yoeli mwana wa Pethueli maana ya jina lake ni “Bwana ni Mungu”. Nyingi ya kumbukumbu zake katika kitabu hiki na huduma yake hekaluni zinaonesha kwamba alikuwa nabii aliyetumwa kwa Yuda na Yerusalemu. Kutokana na huduma yake, wengi wamemdhania kuwa nabii wa “kikuhani” (linganisha Yer 28:1, 5) aliyenena neno la kweli la Bwana.
Tukio hili lilitafsiriwa kuwa ni pigo kwa sababu ya dhambi za watu. Yoeli alilitafsiri tukio hili kuwa ni kielelezo cha ujio wa “siku ya Bwana”, yaani siku ya hukumu. Tukio hili la nzige lilileta maombolezo makubwa katika nchi ya Palestina na kupelekea makuhani kulia kilio kikuu. Hata hivyo, kitabu kinaonesha kuwa tukio la nzige halikuwa neno la mwisho kwani baada ya maombolezo makubwa, watu walifarijiwa kwa kuahidiwa kupata furaha kuu. Akiwaonya watu wamgeukie Bwana kwa toba, Yoeli anatangaza kwamba “siku ya Bwana” inakuja kwa ajili ya hukumu. Lakini Yoeli anaonesha kuwa kabla siku ya hukumu haijatimia, Mungu atatuma Roho wake ili kuleta baraka. Katika tukio la nzige, Yoeli aliona ishara ya hukumu ya mwisho, hivyo akawaonya watu watubu na kumrudia Mungu.
Mwandishi
Yoeli mwana wa Pethueli.
Kusudi
Kuonya Yuda juu ya hukumu ya Mungu iliyokuwa karibu kwa sababu ya dhambi zake; na kuwahimiza watu wamrudie Mungu.
Mahali
Yerusalemu.
Tarehe
Mnamo 835–796 K.K.
Wahusika Wakuu
Yoeli na watu wa Yuda.
Wazo Kuu
Hukumu na kumrudia Mungu.
Mambo Muhimu
Pigo la nzige, kuwaonya watu watubu, na tumaini kwa watu wa Mungu.
Yaliyomo
Kuvamiwa na nzige (1:1–2:17)
Maonyo na baraka za Mungu (2:18–3:12).

Iliyochaguliwa sasa

Yoeli Utangulizi: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia