Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ayubu 36:1-15

Ayubu 36:1-15 NENO

Elihu akaendelea kusema: “Nivumilie kidogo zaidi nami nitakuonesha kwamba yako mengi zaidi ya kusemwa kwa ajili ya Mungu. Ninayapata maarifa yangu kutoka mbali, nami nitamhesabia haki Muumba wangu. Uwe na hakika kwamba maneno yangu si ya uongo; mmoja aliye mkamilifu katika maarifa yuko pamoja na wewe. “Mungu ni mwenye nguvu, lakini hamdharau mwanadamu; ni mwenye nguvu, naye ni thabiti katika kusudi lake. Hawaachi waovu waendelee kuishi, bali huwapa walioteswa haki yao. Yeye haondoi macho yake kwa wenye haki; huwaketisha penye viti vya utawala pamoja na wafalme, na kuwatukuza milele. Lakini ikiwa watu wamefungwa kwenye minyororo, wakiwa wameshikiliwa na kamba za mateso, huwaonesha yale waliyoyatenda, kwamba wametenda dhambi kwa majivuno. Huwafanya wao kusikia maonyo, na huwaagiza kutubu uovu wao. Wakitii na kumtumikia, wataishi siku zao zilizobaki katika mafanikio, na miaka yao katika utoshelevu. Lakini wasiposikiliza, wataangamia kwa upanga, nao watakufa pasipo maarifa. “Wasiomcha Mungu moyoni mwao huficha chuki; hata anapowafunga, hawamwombi msaada. Wanakufa wangali vijana, miongoni mwa mahanithi wa mahali pa ibada za sanamu. Bali wao wanaoteseka huwaokoa katika mateso yao, na kuzungumza nao katika dhiki zao.